Magufuli aagiza wananchi walipwe bilioni 3.4

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
1574685249208.png

Rais John Magufuli ameliagiza Jiji la Dodoma kuanzia Desemba mosi mwaka huu lianze kulipa fidia kwa wananchi wa Kikombo Dodoma ambao maeneo yao yamechukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi Tanzania.

Ametoa agizo hilo leo muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo na amemuelekeza Mkurugenzi wa jiji hilo, Godwin Kunambi atumie shilingi bilioni 3.399/- kuwalipa fidia wananchi 1,509.

Rais Magufuli pia amesema makao makuu ya jeshi ni ya Watanzania hivyo atatoa sh bilioni 10/- za kuanza kujenga makao makuu hayo na tayari alishatoa sh bilioni 5/- za kujengea miundombinu wezeshi kwa ajili ya ujenzi huo.

“Kwa hiyo kuanzia tarehe moja mwaka huu watani zangu wagogo wa maeneo haya ambao wapo 1,500 wanaostahili kulipwa fidia waanze kulipwa fedha zao bila kupunjwa” amesema Rais Magufuli.

Ametoa mwito kwa wananchi waepuke matapeli, wasianze kubadili viwango vya fidia wanavyostahili kulipwa na watakaochelewesha mchakato wa kulipwa itabidi waende kuomba fidia JWTZ.

Ameagiza pia barabara km 18 kwenda kwenye eneo hilo ijengwe kwa kiwango cha lami na mfumo wa dharura na kwamba, zabuni itangazwe kuanzia wiki ijayo na isizidi wiki mbili.

“Na hii ni emergency (dharura) kujenga makao makuu ya Jeshi la Wananchi…mimi nina imani kubwa sana na jeshi letu la wananchi, ni jeshi la kweli, ni jeshi lenye uwezo, ni jeshi linalojitambua, ni jeshi lenye nidhamu, lina makamanda mahiri, lina wapiganaji wazuri wenye nidhamu…nipo pamoja na ninyi sitawaangusha kamwe” amesema Rais Magufuli.

Chanzo: Habari Leo
 
atatoa sh bilioni 10/- za kuanza kujenga makao makuu hayo na tayari alishatoa sh bilioni 5/- za kujengea miundombinu wezeshi kwa ajili ya ujenzi huo.

taasisi ya uraisi barani afrika ina raha sana, ukiwa mzalendo kidogo unaweza kujenga jengo la burj khalifa na usiulizwe chochote
 
I wish I could be general, huyu jamaa angekuwa mwanajeshi tungepata shida sana
 
Analiogopa sana jeshi, kujipendekeza kwingi!
 
Rais John Magufuli ameliagiza Jiji la Dodoma kuanzia Desemba mosi mwaka huu lianze kulipa fidia kwa wananchi wa Kikombo Dodoma ambao maeneo yao yamechukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi Tanzania.

Ametoa agizo hilo leo muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo na amemuelekeza Mkurugenzi wa jiji hilo, Godwin Kunambi atumie shilingi bilioni 3.399/- kuwalipa fidia wananchi 1,509.

Rais Magufuli pia amesema makao makuu ya jeshi ni ya Watanzania hivyo atatoa sh bilioni 10/- za kuanza kujenga makao makuu hayo na tayari alishatoa sh bilioni 5/- za kujengea miundombinu wezeshi kwa ajili ya ujenzi huo.

“Kwa hiyo kuanzia tarehe moja mwaka huu watani zangu wagogo wa maeneo haya ambao wapo 1,500 wanaostahili kulipwa fidia waanze kulipwa fedha zao bila kupunjwa” amesema Rais Magufuli.

Ametoa mwito kwa wananchi waepuke matapeli, wasianze kubadili viwango vya fidia wanavyostahili kulipwa na watakaochelewesha mchakato wa kulipwa itabidi waende kuomba fidia JWTZ.

Ameagiza pia barabara km 18 kwenda kwenye eneo hilo ijengwe kwa kiwango cha lami na mfumo wa dharura na kwamba, zabuni itangazwe kuanzia wiki ijayo na isizidi wiki mbili.

“Na hii ni emergency (dharura) kujenga makao makuu ya Jeshi la Wananchi…mimi nina imani kubwa sana na jeshi letu la wananchi, ni jeshi la kweli, ni jeshi lenye uwezo, ni jeshi linalojitambua, ni jeshi lenye nidhamu, lina makamanda mahiri, lina wapiganaji wazuri wenye nidhamu…nipo pamoja na ninyi sitawaangusha kamwe” amesema Rais Magufuli.

Chanzo: Habari Leo
Jibu utekelezaji mkuu imekwisha hiyo
 
Back
Top Bottom