Tatizo moja tu ambalo Hayati Magufuli alikuwa nalo ni kupenda chama chake cha siasa CCM kuliko nchi ya Tanzania. Hii ilisababisha sana yeye kuangalia maslahi ya chama bila kujali maafa yake kwa taifa na nitatoa mifano michache
1. Kitendo cha kutumia usalama wa taifa kuchunguza wanasiasa wa upinzani ni kusaidia CCM lakini haijanufaisha taifa. Hii imefanya mpaka sasa watu kutokuamini usalama wa taifa badala yake wanaona ni kama chombo cha kisiasa zaidi kuliko kitengo cha usalama wa nchi
2. Kitendo cha kuzuia mikutano ya siasa bila sababu ya kimsingi ya kikatiba nayo imeweka dosari kubwa sana kwenye taifa na kuweka fikra kwa viongozi wajawo wasiheshimu sheria. Huwezi kuwa Raisi wa nchi halafu ukatumia madara yako kufanya vitu vya kunufaisha upande wa chama chako pekee. Msingi wa katiba ni ushindani wa hoja na uchaguzi huru na kama ukiondoa upinzani ni sawa na kukatalia katiba ambayo wewe mwenyewe umeapa kuilinda.
3. Kitendo cha wanasiasa wa wapinzani kupigwa risasi, kubambikwa kesi na hata wengine kupotea. Nchi kama Tanzania na usalama wake huwezi kupigwa risasi bila watu wa usalama kujua! Hii wala halina mjadala Hayati Magu aliweka mbele chama kuliko taifa. Vilevile walishidwa hata kutoa ushahidi wa wale waliopigwa risasi kama kweli walikuwa wanahatarisha taifa! Huwezi kuagiza au kuruhusu watu wauliwe kwasababu tu ni wa vyama pinzani . Hii ni kujali chama zaidi ya taifa.
4 Uchaguzi wa serikali za mitaa na wa mwaka 2020 usalama wa taifa waliutaifisha. Huwezi kitendo cha kuweka wabunge karibu wote wa CCM kwa kuiba na kubadilisha kura bila kujali nchi au hata wananchi kwa manufaa ya chama sio sawa. Mpedwa wetu alikosea hapa na Mungu amsamehe.Sasa kama mbinu ilikuwa kuongezewa muda wa Uraisi Mungu hakutaka hivyo. Na Hii ndiyo maana ni muhimu kufuata misingi na haki maana huwezi kujua kama utakuwepo!
Kuna mengi kafanya mazuri lakini kwenye siasa mpedwa wetu alikosea sana.
Mama ameona hii na ata jaribu kujali nchi kuliko chama hata kama akipata maadui ndani ya chama ilimradi Mtanzania anaendelea