Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Bado nayakumbuka maneno aliyokuwa akiyatamka mara Kwa mara, Rais wa awamu ya 5, Mwendazake John Magufuli kuwa nchi hii ni tajiri sana, ambayo inaweza hata kuwa ni mfadhili wa nchi nyingine, badala ya kuwa Kila siku kuwa omba omba wa misaada.
Nitatoa mifano michache kuthibitisha kuwa nchi yetu siyo masikini kivile, Ila tatizo ni viongozi wetu, katika kupanga vipaumbele vya matumizi.
Kila Rais Samia anapofanya ziara mikoani, anakuwa na misafara mikubwa mno ya magari yasiyopungua 100, ambayo ni matumizi mabaya mno, ambapo ni pesa zetu walipa Kodi wa nchi hii.
Rais anafikia hatua ya kugawa pesa katika mambo ambayo hayana tija.
Rais analipa Kila goli linalofungwa Kwa vilabu ya mpira wa miguu, vinavyoshiriki mashindano ya club bingwa Afrika, goli Moja shilingi milioni Tano, ambazo ni pesa za walipa Kodi wa nchi hii!
Rais anakuwa na Ikulu tatu, ambazo ni Ile ya makao makuu, Dodoma.
Ikulu ya magogoni Dar-es-sdlaam na hiyo ya kizimkazi Zanzibar, ambapo zote hizo Ikulu 3 zinahudumiwa Kwa mabilioni ya pesa ya walipa Kodi wa nchi hii!
Abdul, mtoto wa Rais, Kila siku anatembea na mabulungutu ya pesa za kutaka kuwahonga wapinzani, watakaokubali, kuhama vyama vya upinzani, na kujiunga na CCM, ambazo ni pesa za walipa Kodi wa nchi hii!
Hivi Kwa mifano hiyo michache ya matumizi ya hovyo kabisa za pesa za walipa Kodi wa nchi hii, unategemea kweli maisha ya watanzania yaboreke??
Badala yake ndiyo unakuta maisha ya watanzania, walio wengi yanazidi kudidimia, Kwa msemo wa waswahili, wanasema afadhali ya Jana.
Kitu ambacho nakishangaa zaidi, hayo matumizi yote ya hovyo, hayapangwi na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambalo ndilo lenye mamlaka pekee, Kwa mujibu wa wa Katiba ya nchi, liliopewa mamlaka ya kupanga bajeti ya Kila wizara, Kila mwaka!
Huyo Magu, kasoro yake kubwa ilikuwa ni Moja tu, alikandamiza sana Demokrasia, lakini kiutendaji alikuwa anafanya vizuri sana
Nawaomba wasomaji wengine wa JF, muongezee matumizi mengine ya hovyo, yanayofanywa na hawa watawala wetu