Uchaguzi 2020 Magufuli ametimiza ahadi zake zote kwetu Watanzania kazi imebakia kwetu Wapiga kura hiyo Oktoba 28

Lituye

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
1,864
Reaction score
5,695
Magufuli alituahidi akipata Urais matajiri wataishi kama mashetani. Mpaka sasa matajiri kibao wamefilisiwa mali zao kikatili wengine wamefungwa magerezani bila hukumu ya Mahakama na biashara zimedorola.

Alituahidi pia akiwa Rais wakulima tutalimia MENO. Ameitimiza kwa kupora korosho za wakulima kwa kutumia jeshi bila kuwalipa chochote mpaka sasa. Bei za mazao zimeshuka kupita kiwango Wakulima hatuwezi kununua pembejeo maisha magumu sana na akatoa Ahadi nyingine ya kupiga mashangazi zetu wakulima ambayo hakutuahidi awali.

Kimsingi Ahadi zake ametimiza asubirie tuu hiyo Oktoba 28 na sisi tumfurahishe kweli kweli yaani atafurahi sana.

Atajua kwamba hajui mwaka huu.

Maendeleo hayana vyama.
 
Yaani kuna jirani anajutia kwa nini hakujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura, angeunga juhudi saa 11 asubuhi
 
tapeli huyo hajatoa laptop kwa kila mwalimu laptop na milioni 50 kila jijiji
 
Huyu Mjinga wa kijani tutamnyoosha tareh 28/ 10 mpaka atajua hajui
 
Ili uzi wako udumu JF lazima uandike kichwa kwa style hiyo na content ndio upige spana
 
CCM ni ukoo wa panya—babu mwizi, baba mwizi, watoto wezi, wajukuu wezi, vitukuu wezi, vilembwe wezi na vining’ina wezi! Ukoo huu wa panya walikuwa wanasafiri katika boti la muhogo, lakini kwa sababu ya uroho wao, walianza kulitafuna boti! Kilichofuata ni ukoo mzima wa kizazi cha panya kuzama na kuangamia.

CCM wameanza kuitafuna nchi tangu mwaka 1961 lakini ukomo wao wa kutafuna rasilimali za nchi ni mwaka 2020 kwani hakuna mtanzania mwenye hamu ya kuongozwa na chama cha kifisadi kama CCM ambacho kimeshindwa kuboresha maisha na ustawi wa watanzania. Wananchi wamechoka kubebeshwa ‘magunia ya misumari’ ya bei ya juu ya chakula, mfumuko wa bei wa kutisha, elimu duni, maisha duni, ufisadi wa kutisha na matatizo lukuki yanayosababishwa na panya (CCM) hawa wasiokuwa na haya! Kizazi kizima cha CCM kinakaribia kuzama na kusahaulika kabisa katika ardhi ya Tanzania.
 
Nimependa ubunifu wako ktk kuandika kichwa Cha habari. Umejua kucheza na fitina za mods wa JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…