Magufuli anatupigania WaTanzania. Wengi wetu hatufahamu!

Dah... mbona mnaturusharusha wazeya....mlianza kutabiri wiki ya pili ya March...mkaja kusema wiki ya kwanza ya April tutakiona...mkaja tena May tutaanza kuokotana mabarabarani...Sasa tena leo mnasema mwezi wa 7 [emoji44]
Kuweni siriaz banaaa[emoji41]

Sent using Beretta ARX 160
 
Si mlianza kusema afta tuu wiks?
Naweza kusema jambo moja ila lisiwafanye watu wabweteke.

Inaonekana sasa kwa namna fulani yale yaliyosemwa mwanzoni kabisa kuhusu waafrika na corona pengine yana ukweli fulani. Kwamba virus vya corona vinaweza visiwaathiri waafrika sana kutokana na hali ya hewa Afrika na kinga mwili za waafrika.

Ni kwamba kwa mahesabu (mathematical modelling) ya mwezi February/March ilitarajiwa kuwa hali ya corona ingekuwa ya kutisha mno Afrika ifikapo May yaani sasa. Ila kulingana na taarifa za nchi nyingi bado maambukizi ni machache ukilinganisha na nchi za Ulaya mwezi ilivyokuwa March/April (kumbuka maambukizi yalifika Afrika takriban mwezi mmoja baada ya Ulaya).

Kwa mfano maambikizi yote ya nchi za Afrika ni ~80,000 yaani hayajafikia ya nchi moja tu kwa mfano Peru (88,000 cases). Kama ukiichukua Afrika kama nchi moja basi sasa tupo namba 13 kwa maambukizi, namba 1 ni Marekani yenye visa zaidi ya 1,500,000.

Sababu za hali kutokuwa mbaya kama ilivyotabiriwa:

1. Kiwango kidogo cha upimaji. Nchi nyingi za Afrika zimepima watu wachache sana zikiongozwa na Tanzania
2. Kuficha ukweli. Baadhi ya nchi zinaweza kuficha uhalisia wa mambo (maambukizi na vifo) kwasababu za kisiasa na kiuchumi. Hili linawezekana sana katika nchi zilizo dhaifu na zisizo na demokrasia imara kama ilivyo Afrika
3. Hali ya hewa ya Afrika. Nchi nyingi za Afrika zina joto na unyevu mwingi. Imesemwa hivi karibuni kuwa hali hii hufanya virus visikae kwa muda mrefu kwenye hewa au vitu
4. Matumizi ya dawa za kienyeji. Kuchelewa kwa maambukizi kufika Afrika kumewafanya watu kujiandaa na kuanza kutumia "kinga" za vyakula kama tangawizi, pilipili, vitunguu, malimao na kujifukiza (nyungu). Afrika ina mimea dawa mingi na bado waafrika wengi hutegemea mitishamba hii.
5. Kinga imara dhidi ya magonjwa. Waafrika wa Kusini mwa jangwa la Sahara wanafahamika kwa kuwa na kinga imara ya asili dhidi ya magonjwa mbalimbali. Mafua yanayoweza kumuua mzungu yanaweza hata yasimsumbue mwafrika.

Ila ikumbukwe kwamba maambukizi ya corona Afrika bado hayajafikia kilele (peak) au uwanda (plateau), bado idadi inaongezeka lakini inaonekana kuchukua muda mrefu. Hivyo corona inaweza kubaki Afrika kwa muda mrefu zaidi kuliko sehemu nyingine duniani kwani inaonekana watu wengi hawaoneshi dalili (symptoms) na hivyo huendelea kuambukiza watu wengi zaidi.

Mahali kama Afrika pengine kila mtu ataambukizwa corona wakati fulani ukifika, lakini watakoathirika vibaya ni wachache. Hivyo yawezekana kwamba tukalazimika kuishi na corona kwa muda mrefu hadi chanjo itakapopatikana.
 
Watanzania wa jamiforums pekee ndio Kuna baadh hawafaham kua magufuli anawapigania Ila ingia mitaan ndio utawaona wale wananch wanao faid amri za Rais wao
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shikamana mwenyewe, umesahau alivyotuteka, kutupiga risasi na kutupa kesi zauhujumu uchumi
 
Sawa ila no.2 Hapana,maradhi hayafichiki.Halafu no.1 nilijua utaitaja Tz tu.... Anyway nimekuelewa.
 
Hiyo video inadhihirisha ukweli wa alichoibua Magufuli, usahihi wa vipimo vya corona! Inasikitisha dunia nzima wmekuwa mateka wa hofu ya jinamizi corona bila kuruhusu akili huru kuuliza mantiki ya kila kinachoelezwa kuhusu korona!
 
Unajua idadi ya waliouawa tangu 2016? Azory, Ben saa8, Lwijabe na wale wa kwenye mifuko ya sandarusi wasio na idadi....Tundu Lisu alikoswakoswa adhabu yake ni kumfukuza Ubunge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Katamka uchumi kwanza. Maisha yapi unayoyaongelea wewe?

Katamka hakuna haja ya mabarakoa kinyume cha wataalamu wote wa afya.

Haonyeshi hata kujali kwa kifo chochote. Vita ili anayokupigania? Labda kama wewe ndiye virus mwenyewe wa Corona.
 
Hivi kwa dunia ya sasa mtu bado unafuata muongozo elekezwa..kila mtu sasa hivi anajua Korona ni nini, inaambukizwaje, tunaweza kujikinga vipi....hivyo sasa hivi hatujali serikali inasema nn....au Magu anasema nn....sasa hivi ni mwendo wa barakoa, vitakasa mikono, kupunguza safari , kukaa mbalimbali.....Hivo kila mtu anapambana na hali yake....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulitoroka na kuji-lockdown tukitaraji waliobaki mjengoni watapukutika. 14deis zimekwisha, tunajipanga upya tutoke vipi na Oktoba'20 inakaribia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…