Magufuli awaumbua mastaa...

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801


Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.


KUFUATIA kuwepo kwa makundi yaliyotokana na watangaza nia 42 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliokuwa wakiwania nafasi ya urais, mastaa waliokuwemo ndani ya makundi hayo wameumbuka kufuatia ushindi wa John Pombe Magufuli, Risasi Mchanganyiko lina ‘full' stori.

WAMEUMBUKAJE?
Listi ndefu ya mastaa ikiongozwa na Jacqueline Wolper, Wema Sepetu ‘Madam', Wastara Juma, Kajala Masanja, Elizabeth Michael ‘Lulu, Vincent Kigosi ‘Ray', Jacob Stephen ‘JB', Bahati Bukuku, Tunda Man, Diamond na wengineo walikuwa wamegawanyika, baadhi wakimuunga mkono Bernard Membe na wengine Edward Lowassa hivyo alipopitishwa Magufuli ambaye hakuwa na wapambe, wakajikuta wameumbuka.
.

CHANZO CHASHUSHA UBUYU
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na mastaa hao, kuumbuka kwao kulikuwa kwa aina mbili. Kuna baadhi walikwenda Dodoma kulipokuwa kukifanyika vikao vya kuwachuja wagombea wakiwa wamejiandaa kwa sherehe lakini kuna ambao walibaki Dar kusikilizia."Walikwenda Dodoma wakiwa wameshahakikishiwa ushindi wa Membe na Lowassa, lakini bahati mbaya kwao hakukuwa na yeyote kati yao aliyefanikiwa kupenya, ingawa Membe aliingia Tano Bora," kilisema chanzo chetu.

KIZINGITI KILICHOWAKWAMISHA
Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani, jina lake halikufanikiwa kuvuka kwenye Kamati Kuu huku Membe ambaye ni Mbunge wa Mtama akiienguliwa katika mkutano wa Halmashauri Kuu.WALITINGA DOM KWA MBWEMBWEChanzo kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, mastaa hao walitinga Dodoma kwa mbwembwe ikidaiwa kuwa walishahakikishiwa ‘mtonyo' baada ya mgombea wao kushinda."Ilikuwa wameshahakikishiwa ulaji. Wagombea wao waliposhindwa kuvuka, posho zao nazo zikayeyuka papo hapo."

KUMBE WALIANDALIWA SARE"
Yani ishu ilikuwa ni kubwa. Unaambiwa waliandaliwa hadi sare kwa ajili ya kusherehekea ushindi lakini mambo yote yaliharibika baada ya wagombea wao kushindwa," kilieleza chanzo hicho na kuongeza:"Yaani waliumbuka kwelikweli maana kuna ambao hawakwenda Dodoma lakini walikuwa wamewakilishwa na wenzao walioenda na mikakati yao ilikuwa wangepita wagombea wao, wangeungana kuwapigia kampeni nchi nzima.

WASIOKWENDA DODOMA
Risasi Mchanganyiko limechimba wasanii ambao wanadaiwa kutokwenda Dodoma na kutajwa kuwa wamewakilishwa na wenzao huku wakipiga kampeni kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni pamoja na Jacqueline, Wema, Lulu, Kulwa Kikumba ‘Dude', Bahati Bukuku na Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA'.

WALIOENDA DODOMA NI KINA NANI?
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa, miongoni mwa wasanii waliokwenda Dodoma na kudaiwa kujipanga kwa sherehe hizo za ushindi wa makundi ya wagombea ni pamoja na Steven Mengere ‘Steve Nyerere', JB, Kajala, Ray na Wastara.

STEVE NYERERE AFUNGUKA
Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Steve Nyerere ambaye alikanusha kuwepo kwa sherehe iliyopangwa lakini aliungana na wenzake waliokwenda kumuunga mkono Membe lakini kwa kuwa hakushinda, wamehamia kwa Magufuli.

"Sisi hatukuandaliwa sherehe, mimi JB, Kajala, Ray na Wastara tulikwenda kumuunga mkono Membe na tulipewa chetu, sasa kwa kuwa mgombea wetu ameshindwa tulihamia kwa Magufuli ambaye ni timu moja na Membe," alisema Steve.


Chanzo: GPL

 
Asante mkuu..yale nje unakuta "WAZIRI ABAKA"soma ukurasa wa 7...ukienda ukurasa wa 7 unakuta ooh Mkazi wa mbagala Waziri juma amebaka..:what::what:yanatia kinyaa..

Hahahaa yan ni shidaa
 
Hakuna nilichoona zaidi ya tatooo ya lulu.
Mleta mada ujumbe wako umenifikia
 
Asante mkuu..yale nje unakuta "WAZIRI ABAKA"soma ukurasa wa 7...ukienda ukurasa wa 7 unakuta ooh Mkazi wa mbagala Waziri juma amebaka..:what::what:yanatia kinyaa..

Hahahaaaaa...eti waziri abaka...hii kali, halafu wanakuwekea na picha ya mawaziri kumbe haihusiani
 
Hahahaaaaa...eti waziri abaka...hii kali, halafu wanakuwekea na picha ya mawaziri kumbe haihusiani

Hahaha...au unakuta mbele kabisa "MWINYI AFUMANIWA"asa kurupuka ulinunue...ukilisoma utajuta mkuu!
 
Ulimbwende na siasa wapi na wapi. jk kakomesha kwa kuweka bulldozer. wauza sura sasa hakuna uongozi,..kazi tu sasa.
 
Ndio maana ukaitwa UDAKU..., kusoma haya magazeti sio tu kupoteza pesa bali na muda wako pia
 
Mi niliwadharau Membe na Lowassa mara tu walipokusanya hawa wasanii wababaishaji kuwa katika makundi yao ya kampeni.. Watu wenyewe hawajielewi afu unawapa kipaumbele, lazima wenye nchi wakukate tu maana hakuna jinsi.
 
Wasanii amabao hawajawahi ingia ikulu kipindi cha mkulu basi watapasikia kwenye bomba
 
Udaku bhana eti! Rais afanya kufuru ningeria uk..9! ...ukienda ukurasa wa tisa utakutana na Rais wa wasafi Daimond Platnumz afanya kufuru ningeria hell
 
Hapo kwa Mwana FA sio kweli, FA ni team Makamba
 
Yaani hawa wasanii hawafai Hata mmoja ...CCM wasiwapitishe hata mmoja wote wamekimbilia kwenye siasa.
 
Kuna jingine liliwahi kuandika Chelsea yaelekeza juhudi kwa Yanga, kufungua ndani kumbe mchezaji Yanga Mbia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…