Kelvin Kihiyo
New Member
- Nov 13, 2018
- 2
- 1
UTENDAJI kazi wa marais, Dk John Magufuli na Paul Kagame wa Rwanda unaoweka mbele maslahi ya nchi na wananchi umemvutia Balozi wa Rwanda nchini, viongozi hao ni mfano wa kuigwa. Utendaji wa marais hao, unaojali zaidi vitendo vyenye kuonyesha matokeo chanya badala ya maneno yasiyo na tija, ndiyo kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kasi katika nchi zao. Utashi wa kisiasa walionao umeimarisha zaidi uhusiano na biashara baina ya mataifa hayo mawili ya Afrika Mashariki. Uongozi wa Rais Kagame na wa Rais Magufuli unajali zaidi maslahi ya wananchi na kuweka nguvu katika vitendo, badala ya maneno, kuimarisha mahusiano na kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji biashara na hiyo ndiyo siri kubwa ya kukua kwa uchumi wa mataifa hayo.
Katika sekta ya usafirishaji wa mizigo, Rwanda inatumia zaidi Bandari ya Dar es Salaam, akieleza kuwa zaidi ya asilimia 90 ya bidhaa zinazotumiwa nchini humo kutoka na kwenda nje ya nchi hiyo, zinapitia Tanzania. Kuimarika kwa biashara kati ya nchi hizi mbili kunasababishwa na utashi wa kisiasa walionao viongozi wa mataifa haya ambao Julai 2016 walikubaliana kuimarisha uhusiano wa kibiashara.
Miongoni mwa mambo yanayoimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili ni pamoja na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kufungua tawi jijini Kigali na Mamlaka ya Mapato Rwanda (RRA) kufungua tawi bandarini jijini Dar es Salaam. Uwepo wa maofisa wa TPA nchini Rwanda na wa RRA jijini Dar es Salaam umerahisisha sana mambo mengi ambayo yamechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha biashara na uwekezaji na umesaidia changamoto zinapoibuka kupatiwa ufumbuzi wa haraka papohapo tofauti na hapo awali
.
Hata hivyo, wafanyabiashara wa Tanzania, wamewekeza zaidi Rwanda kuliko wa Rwanda walivyowekeza Tanzania. Karibu kampuni 15 za Tanzania zimewekeza nchini Rwanda na moja ya kazi za Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, itakuwa ni kuhamasisha wafanyabiashara wa nchi yake nao kuja kuwekeza kwa wingi Tanzania. Aidha, kuimarika kwa uhusiano wa kibiashara na uwekezaji, umesaidia kuimarisha usafiri wa watu na usafirishaji mizigo kutoka Kigali hadi jijini Dar es Salaam, ambapo ndege ya Rwanda Air imekuwa ikileta Tanzania wafanyabiashara wengi kila siku. Shirika la Ndege la Rwanda limeendelea kustawisha uhusiano kati ya nchi hizi mbili kwa kuwa na safari za Kigali kuja Dar es Salaam, hali kadhalika kutoka Dar es Salaam kwenda Kigali kila siku.
Kuhusu usafiri wa barabara, umeimarika kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwapo kwa usafiri wa mabasi ya Trinity kutoka jijini Kigali hadi Dar es Salaam kila siku hivyo kuchagiza ufanyaji biashara baina ya wananchi wa mataifa hayo mawili. Hayo yote yanatajwa kuwa ni mafanikio makubwa yaliyosababishwa na kuimarika kwa uhusiano kati ya Tanzania na Rwanda. Katika kuimarika zaidi uhusiano kati ya Rwanda na Tanzania, Juni mwaka huu kulifanyika mkutano mjini Kigali wa mawaziri wa biashara wa Tanzania na Rwanda ulioangalia namna ya kuimarisha mazingira ya biashara kati ya mataifa hayo mawili. Alisema matunda ya mkutano huo yalionekana Oktoba mwaka huu, ambapo Rwanda ilizindua bandari kavu ya kutunzia mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam.
Miongoni mwa mambo ambayo serikali zilikubaliana kwa dhati ni utendaji mzuri katika vituo vyetu vya mpakani, ambapo tulikubaliana kufanya kazi kwa saa 24 ili kurahisisha biashara baina yetu.
Rwanda imevutiwa na utendaji wa Rais Dk Magufuli ambao umeweka mazingira mazuri ya biashara baina ya nchi hizo, kufanyika bila matatizo yoyote. Bandari ya Dar es Salaam, imekuwa kama moyo wa uchumi wa Rwanda kutokana na bidhaa nyingi za nchi hiyo kutoka na kwenda nje ya nchi kupita bandarini hapo. Muda wa kuchukua mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam kwa sasa umepungua kwa kiasi kikubwa kutoka siku saba hadi moja au mbili, hili ni jambo zuri sana. Kutokana na kupungua kwa muda wa kutoa mizigo bandarini, muda wa kusafirisha mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam hadi jijini Kigali umepungua vilevile kutoka siku tisa hadi siku tatu.
Zamani kulikuwa na usumbufu njiani kwa kuwa na vituo vingi vya kupima uzito wa magari na wakati mwingine kulikuwa na matumizi ya rushwa, lakini tangu Rais Magufuli aingie madarakani vituo hivyo vimepunguzwa hadi kufikia vitatu na ufisadi umepungua kwa kiwango kikubwa. Kwa sasa Tanzania kuna idadi kubwa ya wafanyabiashara kutoka Rwanda kuliko wakati mwingine wowote na kwamba hiyo inatokana na mazingira rafiki ya kibiashara yaliyojengwa baina ya mataifa hayo mawili.
hali hiyo, imesababisha kampuni kubwa za Rwanda kutaka kuja kuwekeza Tanzania mfano kampuni moja ya nchi hiyo kupanga kuja kuwekeza katika sekta ya maji. Aidha, katika kuhakikisha uhusiano wa kibishara na uwekezaji, unazidi kukua baina ya Tanzania na Rwanda, nchi hiyo ipo katika mkakati wa kuitisha jukwaa la biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili.