Magufuli kuwa Rais wa kwanza Tanzania utawala wake chuki kutawala katika jamii?

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Nawasalimu, amani iwe juu yenu wanajukwaa!

Naapa kwa aliyeumba, huyu ataenda kuwa Rais ambaye atavunja historia tangu nchi hii ipate uhuru watu wataishi katika Chuki na visasi vya hapa na pale. CCM kitakua ndicho chama kitakachochukiwa na watu wote katika jamii na hata wao watachukua na wenyewe kwa wenyewe.

Mtaani CCM kitakosa heshima, litaonekana kama chama cha mabavu, chama cha wenye uchu na madaraka, chama kisichojali maamuzi ya wananchi.

Magufuli amedanganywa wa washauri wake kwamba kubakiza Chama tawala bungeni 99% ndiyo suluhisho la matatizo ya nchi hii. Wenye kuelewa maana ya utawa hufanya kazi kwa kushirikiana na mahasimu wao.

Sasa CCM wanataka wafanye kazi bila serikali kukosolewa wala kunyooshewa kidole. Sasa na tuone watafika wapi, hili litakua bunge litakalochukiwa kuliko mabunge yote duniani.

Dhambi haidumu milele na Mungu hua hadhihakiwi.
 
JK alitenda mema yote bado akachukiwa, wapinzani kweli hawana jema.
 
Watu Wana Hofu
Wachambuzi Wanasifia, Radio, Television
 
Namshukuru sana Mungu wangu kwa kutoshiriki kwa namna yoyote ile kwenye haya maigizo.
 
Allaniwe anaepandikiza mbegu ya chuki kwa taifa letu. Tutajuta pamoja maisha yatakuwa magumu zaidi, japo huenda Mola analake kuwapa kiburi watawala ili hasira za wengi zitamalaki.
 
Tatizo watu wanaamini mtu anashinda kwa kuongopeana mitandaoni. Hongera Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, unaelekea kushinda kwa kishindo
 
Bunge litakuwa la kipuuzi kuliko yote yaliyowahi kutokea kwenye historia ya nchi hii, na Spika wake akiendelea kuwa Ndugai ndio litakuwa la hovyo zaidi, sitashangaa wakiendelea kuijadili Chadema bungeni.
 
Tatizo watu wanaamini mtu anashinda kwa kuongopeana mitandaoni. Hongera Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, unaelekea kushinda kwa kishindo
Wacha kujidanganya mwizi mkubwa.
 
Ambacho ni obvious kabisa ni kua marafiki zake wa karibu wote watatajirika mno maana kazi zote za serikali zitakua zinafanywa na kampuni zao, ukiwa nje ya circle sahau kupokea tender hata moja...
Umeongea point muhimu sana,

Kua sasa kutakua hakuna wa kumlaumu kua flan ni upinzan ameshindwa kuleta maendeleo, flan ametumwa na mabeberu ndio mana maendeleo hamna, sasa tunatarajia Tanzania itakua ulaya ndogo, Dar itakua kama beijing, Arusha itakua kama geneva uswisi, tabora kama toronto, Kilimanjaro kama Spain, wananchi watakuwa matajiri.
 
Ukishikamana na shetani, nawe ni sehemu ya shetani.

Binafsi, nitabakiza uhusiano wa kawaida na wanaCCM lakini siyo urafiki wala ukaribu. Kuwa na urafiki na mwanaCCM ni kujitia unajisi.

Maandiko yanasema, mkono wako ukikukwaza, ukate, uutupe. Jicho lako likikukwaza, ling'oe ulitupe. Maana ni aheri kuingia mbinguni ukiwa na mkono mmoja kuliko kubakia na viungo vyote halafu ukaukosa ufalme wa mbinguni.

Viungo vinavyokwaza ni nini? Ni marafiki wabaya, tawala mbaya, tamaa mbaya, na mazingira yote yanayokufanya utende dhambi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawasalimu, amani iwe juu yenu wanajukwaa!

Naapa kwa aliyeumba, huyu ataenda kuwa Rais ambaye atavunja historia tangu nchi hii ipate uhuru watu wataishi katika Chuki na visasi vya hapa na pale. CCM kitakua ndicho chama kitakachochukiwa na watu wote katika jamii na hata wao watachukua na wenyewe kwa wenyewe.

Mtaani CCM kitakosa heshima, litaonekana kama chama cha mabavu, chama cha wenye uchu na madaraka, chama kisichojali maamuzi ya wananchi.

Magufuli amedanganywa wa washauri wake kwamba kubakiza Chama tawala bungeni 99% ndiyo suluhisho la matatizo ya nchi hii. Wenye kuelewa maana ya utawa hufanya kazi kwa kushirikiana na mahasimu wao.

Sasa CCM wanataka wafanye kazi bila serikali kukosolewa wala kunyooshewa kidole. Sasa na tuone watafika wapi, hili litakua bunge litakalochukiwa kuliko mabunge yote duniani.

Dhambi haidumu milele na Mungu hua hadhihakiwi.
Hii ndiyo inaitwa demokrasi - leo hawa wengi, kesho 50/50, kesho kutwa wachache! Hivyo usilalamike
 
Ukishikamana na shetani, nawe ni sehemu ya shetani.

Binafsi, nitabakiza uhusiano wa kawaida na wanaCCM lakini siyo urafiki wala ukaribu. Kuwa na urafiki na mwanaCCM ni kujitia unajisi.

Maandiko yanasema, mkono wako ukikukwaza, ukate, uutupe. Jicho lako likikukwaza, ling'oe ulitupe. Maana ni aheri kuingia mbinguni ukiwa na mkono mmoja kuliko kubakia na viungo vyote halafu ukaukosa ufalme wa mbinguni.

Viungo vinavyokwaza ni nini? Ni marafiki wabaya, tawala mbaya, tamaa mbaya, na mazingira yote yanayokufanya utende dhambi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Who cares, kafie mbali
 
Back
Top Bottom