Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Ngurdoto ilikua/ipo chini ya The Impala Group of Hotels (IGH) ambayo ilikua ina jumuisha Impala Hotel (Arusha), Impala Hotel (Moshi), Ngurdoto Mountain Lodge (Arusha), Naira Springs Hotel (Arusha), Impala Shuttle Services (Arusha) na The Classic Tours and Travels.
IGH ilikua inamilikia na marehemu Faustine Meleo Auye Mrema, mzaliwa wa Rombo, Kilimanjaro aliefariki July ya mwaka 2017. Hoteli yake ya kwanza ya Impala alifungia 1988.Biashara kubwa ya Ngurdoto ilikua mikutano ya kiserikali na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa ilikua inafanyika Ngurdoto wakati wa awamu ya nne. Ilipoingia serikali ya awamu ya tano biashara hiyo kutoka kwa serikali na mikutano ya kimataifa ilipungua.
Mwaka 2016 ulifanyika kikao cha wakuu wa nchi wa Jumuiya ambapo Hayati Magufuli akalalamika kuhusu gharama za mkutano huo.Unaweza fungus link hii kwa reference ya baadhi nilisema hapo juu.
Baada ya kukosa mikutano ya kiserikali na kimataifa ndio biashara ikaanza kudorora. Na kama wewe ni mjuzi wa mambo kafuatilie chimbuko la Ngurdoto kuanzishwa.Sasa tufast forward (tusogee mbele) hadi awamu ya sita.
Kaingia Raisi Samia na serikali imeanza tena kutumia hizi facilities binafsi kwa ajili ya mikutano mbalimbali. Hivyo kusema Ngurdoto ilidorora kwa sababu ya kukosa watalii na biashara imerudi kwa sababu ya watalii sio kweli. Kwani Tanzani haijawahi kupungukiwa na watalii ukiacha wakati wa COVID-19 2020/21. Mwaka 2017 Ngurdoto iliamuliwa na Mahakama iuze mali zake kuwalipa wafanyakazi 93 TSh milioni 129.
Mwaka huo huo Tanzania ilikua na watalii wa kigeni 1,327,000. Mwaka 2022 Tanzania ilikua na watalii wa kigeni 1,454,920. Utasemaje mwaka 2017 biashara ya Ngurdoto ilidorora kwa sababu ya watalii na kwa sasa imerudi kwa sababu ya watalii? Na hata The Citizen siku tatu zilipo pita imeandika makala yenye kichwa hiki cha habari.
Kiuhalisia Mrema alikua na wake kadhaa. Na kila mke ni kama alimpa himaya yake ya kumanage. Baada ya Mrema kufariki kulitokea mgogoro wa kifamilia kuhusu nani atarithi nini. Oct mwaka huu Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Arusha ilitengua wasimamizi wa mirathi kwenye kesi ilioisha 2017.
Akateuliwa mtoto wake Randle Mrema kuwa msimamizi wa mali.Kwa hiyo tangu 2017-Oct 23 kulikua na kesi ya mirathi hivyo hoteli isingeweza kuuzwa. Ila baada ya shauri hilo la Oct 23, Randle alieteuliwa kuwa msimamizi wa mali aliongea na vyombo vya habari na akasema atafanyia kazi kulipa madeni na kufufua biashara zilizo kufa. Hivyo sidhani kama kati ya Oct-Nov watakua wameiuza hiyo hoteli. Bado iko chini ya familia ya Mrema.