Tetesi: Magufuli na awamu iliyoua Biashara: Ngurdoto, Impala, Naura, Tours, Warithi waapa kuirudisha: Awamu 5 ilifilisi

JPM alikuwa na ujasiri wa hali ya juu mpaka akawa mfano wa maamuzi magumu haswa kutoka kwenye media za nje.

Humo humo kwenye kuja na maamuzi magumu alizidisha kiburi ikawa ni kama vile anaonewa baadhi ya matajiri akiwa na unyonge wa maisha aliyoishi huko nyuma.

Samia ameingia na diplomasia ya msamaha na inaonekana anataka kuwa rais mpaka 2030 hivyo ametambua kuwa adui wa leo haraka sana anaweza kuwa rafiki wa kesho halafu keshokutwa akaja kuwa adui mbaya kuliko alivyokuwa juzi.

Amejua namna za kujishusha kisiasa na kutafutwa kuungwa mkono na wenye uwezo kwa maana ya matajiri.
 
Acha ujinga na ficha ujinga wako. Hicho kilikuwa kichaka cha kutakatisha hela. Wangekuwa wanajiendesha kibiashara wala wasingekwama. Kumbuka hata Moro kulikuwa na mfanyabiasha mchaga jambazi aliyekuwa anapora vitu vya watu na kufungua maduka kwa kuwapa wachaga wenzie na ilijulikana wachaga ni wafanya biashara maarufu sana hapo Moro ila alipofariki tu wachaga wote walishapoteq morogoro ni waha for now ambao walikuwa wanafanya biashara kwa haki. So Ngurudoto and the like ni magenge ya waharifu yamejengwa kwa hela za wizi na yanatumika kujustify wizi, ikija awamu nyingine watafungiwa tena tu kama hawajirekebisha
 
Hakuna nchi Inaendeshwa kishikaji! Sehemu kubwa ya Wabongo magumashi ni mengi! Hao unaowaita matajiri wengi ni matajiri uchwara tu!
Bakharesa 2015 alianza kujenga hotel yake Verde Zanzibar na baadae 2020 akaanza ujenzi wa bagamoyo Sugar!
Mbona hakufirisiwa?
Hao unaodai sijui wa Kaskazini ni uongo na ukabila ndo unawasumbua!
 
Hao jamaa wanaonga wengine ni wajinga! Hata Tai Five Mwanza 2016 Mchaga alikopa na akashindwa kulipa mkopo ikanunuliwa na Mmiliki wa mabasi ya BATCO!
Hapo napo Magufuli anahusika kutolipa mkopo!
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni,kwa maelezo yako,hotel ziliyumba kwa kukosa deals za serikali wakati wa Maghu!sasa hiyo ni pesa ya umma, Kodi, kama raisi anaona kufanyia mkutano kwenye kumbi za wizara ni nafuu kuliko hotel yako, ubaya upo wapi?
Huwezi kulazimisha watu wakulipe richa ya kwamba unawapiga parefu.
 
Huwezi kumkwepa tajiri maishani mwako. Kuupata utajiri ni changamoto ya wengi na wanakuwa ni wachache kwa sababu ya vigezo vyenye kuwatofautisha.

Inawezekana kuwa matajiri wengi tulionao wana tabia za hovyo lakini busara sio kuwachukia ni kuangalia huo udhaifu walionao na namna ya kuufanya usiwe wa kudumu.

Hauwezi kuiondoa roho ya kutafuta utajiri kwa kuwakomoa matajiri wachache unaokuwa nao kwa wakati husika, sana sana utawatia umaskini wa kudumu masikini walio wengi na unaweza kuangamiza kabisa Taifa likaingia vitani na katika ufukara wa kudumu.
 
Kwa hiyo wewe unaamini Kabisa hiyo hotel sababu ya Kusimama operation ni Utawala wa Magufuli?
 
Ndo maana halisi ya mzunguko wa pesa lazima hotel zipate viongozi wa serikali ili kuwa na cash flow nzuri. Sasa zikifungiwa zinakuwa na kazi Gani zaidi ya wachache kuziiba tu kama walivyokuwa wakifanya akina makonda na sabaya waliokuwa wanajichotea tu. Makonda ni billione na ubillionare kaupata enzi za jpm
 
Si kweli, kwani hakukuwa na PCCB,TISS, TRA na wengineo?
Imeshushwa na wivu wa JIWE na mzee alipofariki sasa ndio msimamizi wa mirathi annaza kuifufua .
 
Mrema alitia ajira kwa wengi sana sana

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…