Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Mke wangu aniamsha, usiku saa sita,
Machozi aomboleza, simu anonyesha,
Habari mbaya napata, usingizi unakata,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Tarehe kumi na tano, ndoto ninaota,
Aniijia Raila Amolo, machozi analia,
Dola toa tangazo, tarehe kumi na saba,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Komandoo JPM, umekufa kwa moyo,
Amiri Jeshi JPM, umekufa kwa moyo,
Kamanda JPM, meondoka kwa moyo,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Tawezamaliza shairi, swali najiuliza,
Msiba ajenda itabadili, toka Corona?
Kukatika mpini, so mwisho kujenga,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Vitabu bado printi, nilivyomuandika,
“Silaha 7 za Magufuli” bado kuchapa,
“Dira ya nchi na Magufuli” bado pia,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Magufuli ni utitiri, aliyembeba tembo,
Lienda ya duma kasi, lileta maendeleo,
JPM umejenga nchi, pasina upendeleo,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Lumumba limwambiaje, natamani jua,
Maalim limwambiaje, natamani kujua,
Obasanjo limwambiaje, natamani jua,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
TB Joshua analia, Magufuli hatunaye,
Malasusa analiaa, Magufuli hatunaye,
Kardinali analiaa, Magufuli hatunaye,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Bagonza na Munga, JPM mlimpenda,
Kilaini na Nyaisonga, JPM limpenda,
Mwingira na Shoo, JPM mlimpenda,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Kitima omboleza, Ruwaichi omboleza,
Niwemugizi alia, Masheikh omboleza,
Upendo mlimpa, BWANA atawalipa,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Babangu Hezbon, Doris mamangu,
Swali wananiuliza, nini mwanangu?
Magufuli amekufa, uuuwiii Mungu!
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Kaushwe mwili, zikwe kaburi la wazi,
Makumbusho jama, jengee Magufuli,
Kijijini kwao Mlimani, Chato wilayani,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Enzi zako Magufuli, FFU ilipumzika,
Enzi zako Magufuli, chinga pumzika,
Enzi zako Magufuli, mamantilie tulia,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Majambazi likizoni, wakati wako JPM,
Mavibaka likizoni, wakati wako JPM,
Mafoleni likizoni, wakati wako JPM,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Umeme bwerere, wakati wako Pombe,
Maji pia bwerere, wakati wako Pombe,
Mitandao huree, wakati wako Pombe,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
King’ongo ulijenga, ndani ya siku sita,
Chini ya mti wasoma, mtandaoni liona,
Ulitoa amri siku saba, ukingali Kahama,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Shujaa wa Uviko, Magufuli ameenda,
Katuachia kiboko, rais Suluhu Samia,
Mbele pambano, muenzi JPM shujaa,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Magufuli ni Nabii, maono alipewa,
Corona iko njiani, ukaliandae taifa,
Weka huduma za jamii, lipone taifa,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Usifunge mipaka, JPM aliambiwa,
Mataifa yatakuijia, wapate kupona,
Usizuie ndani wana, Tz inaponywa,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Kama Yohana Mbatizaji, JPM likuja,
Kumsafishia mahali, Suluhu Samia,
Njiani watu wengi, ka nzige jani wala,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Bilioni tatu unusu, ni nusu ya dunia,
Asema waziri mkuu, wamombolezea,
Amini msiba huu, JPM rekodi avunja,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Marais kumi na saba, JPM wamezika,
Hawakuijali Corona, inayotesa dunia,
Wamejali tu mahaba, JPM aliyowapa,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Jamani Janet ataliaje, albino wataliaje,
Suzi mamake ataliaje, watoto walieje,
Elimu bure taliaje, watekamaji taliaje,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Wastaafu wataliaje, wakulima walieje,
Wavuvi wataliaje, wafugaji wataliaje,
Wajawazito wataliaje, elimu ya juu je?
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Macho mekundu pia, uuaji meondoa,
Wafugaji na wakulima, vita meondoa,
Za utotoni mimba, vita umeimarisha,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Pombe njaa ulifuta, ujambazi ulifuta,
JPM wavivu ulifuta, wapigaji ulifuta,
Kibiti ugaidi futa, ukajenga viwanda,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Viongozi wenzio, marais waliostaafu,
Wapunga upepo, hawana usumbufu,
Uliwaenzi wenzio, atakulipa Mungu,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Majini tuko vizuri, angani tuko vizuri,
Umeachia nchi meli, nchi yote eapoti,
3500 km za lami, zafika Oman nchini,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Treni nchi nzima, ya wese mabomba,
TBC nchi nzima, umeme nchi nzima,
Afya nchi nzima, shule umetapakaza,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Rada nchi nzima, Burundi na Rwanda,
Zao ndege zaongozwa, toka Tanzania,
JPM alama umeacha, ndani kimataifa,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Sadaka ulikusanya, uchafu likusanya,
Michango ulikusanya, kodi likusanya,
Mabandani ulikula, ubugobugo lipiga,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Mikutano ulivamia, pasina kualikwa,
Ulibadili mijadala, lilenga kupata tija
Maslahi ya umma, mbele litanguliza,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Burundi lipatanisha, Sudan patanisha,
DRC ulipatanisha, Kenya lipatanisha,
Rwanda lipatanisha, Zenji lipatanisha,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Malawi tegemea meli, DR Congo pia,
Burundi tegemea meli, nayo Zambia,
Kisumu tegemea meli, nayo Uganda,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Comoro tegemea, ndege za Tanzania,
Maziwa Makuu pia, bandari tegemea,
Sehemu ya Afrika, hospitali tegemea,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Kinematics potea, Pythagoras potea,
Logarithms potea, Quadratics potea,
Kemikali potea, Quantitatives potea,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Wasomi uliteua, hukutumbua pasaka,
Misikiti ulijenga, BAKWATA swalia,
Jemedari nenda, Amiri Jeshi tangulia,
Komando nenda, Kamanda tangulia,
WAPO kazike Chato, FGBFC kazike,
AGAPE kazike Chato, EAGT kazike,
TAG kazike Chato, GRC pia mkazike,
Magufuli alituhimiza, ibada tuishike.
Samia ambie wapigaji, ehiii baghosha,
Samia ambie mafisadi, ehiii baghosha,
Samia ambie walaghai, ehiii baghosha,
Samia ambie maghaidi, ehiii baghosha.
Tarehe kumi saba, JPM sikukuu yake,
Miaka ataenziwa, ka shujaa wengine,
Pombe shujaa, kongamano andaliwe,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Utamu wa Magufuli, ule wake ukali,
Utamu wa pilipili, ni ule wake ukali,
Wampenda wahisani, fedha lidhibiti,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
John hesabu peleka, mbele ya waasisi,
Wa yetu Tanzania, Nyerere na Abedi,
Aambie Tanzania, ni uchumi wa kati,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
JPM salimia Mandela, salimia Aristotle,
JPM salimia Plato pia, salimia Moringe,
Pombe Newton salimia, salimia Socrate,
Magufuli Marx salimia, salimia Nyerere.
John salimia Odinga, salimia pia Stalin,
John salimia Mao pia, na Chirwa Orton,
John sabahi Fidel pia, na Katabalo Stan,
JPM Gandhi salimia, Mkapa na Tubman.
JPM Sankara salimia, Olympio salimia,
JPM Nasser salimia, Anwar pia salimia,
JPM Luthuli salimia, Nkrumah salimia,
JPM Lenin salimia, Ceausescu salimia.
JPM habari pelekee, hao wote wajamaa,
Waambie dunia ile, sasa ni kijiji kimoja,
Eti Mabeberu wote, wakaa na Wajamaa,
Mabeberu wenyewe, ndiyo wanawekeza.
Misahafu ingekuwa, inaandikwa hii leo,
Magufuli ungekuwa, na maandiko yako,
Stalin pia aliijenga, Urusi miaka mitano,
Tubman pia aliijenga, Liberia hivohivyo.
Ulilala saa kumi, kwa ajili ya Tanzania,
Saa Kumi na mbili, Magufuli uliamka,
Ka yule Ujerumani, Bi Merkel Angela,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
University of Magufuli, Chato wekeni,
Kumuenzi jemedari, fundishe kozi hii,
Uongozi mkakati, na ubunifu mkakati,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Tulie kwa tumaini, sijemkwaza Mungu,
Tulie kwa tumaini, sijemkwaza Mungu,
Tulie kwa tumaini, sijemkwaza Mungu,
JPM utafufuliwa, katika kiama ya wafu.
Tanga ninaanua, tutaonana Paradiso,
Twonane Paradiso, twonane Paradiso,
Twonane Paradiso, penye mji wa raha,
JPM tafufuliwa, katika kiama ya wafu.
Jina kamili la Mtunzi ni: Douglas O. Majwala.
Jina la Ushairi ni: The Rod of Grace/Fimbo ya Musa.
majwalaoriko@yahoo.co.uk
Machozi aomboleza, simu anonyesha,
Habari mbaya napata, usingizi unakata,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Tarehe kumi na tano, ndoto ninaota,
Aniijia Raila Amolo, machozi analia,
Dola toa tangazo, tarehe kumi na saba,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Komandoo JPM, umekufa kwa moyo,
Amiri Jeshi JPM, umekufa kwa moyo,
Kamanda JPM, meondoka kwa moyo,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Tawezamaliza shairi, swali najiuliza,
Msiba ajenda itabadili, toka Corona?
Kukatika mpini, so mwisho kujenga,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Vitabu bado printi, nilivyomuandika,
“Silaha 7 za Magufuli” bado kuchapa,
“Dira ya nchi na Magufuli” bado pia,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Magufuli ni utitiri, aliyembeba tembo,
Lienda ya duma kasi, lileta maendeleo,
JPM umejenga nchi, pasina upendeleo,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Lumumba limwambiaje, natamani jua,
Maalim limwambiaje, natamani kujua,
Obasanjo limwambiaje, natamani jua,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
TB Joshua analia, Magufuli hatunaye,
Malasusa analiaa, Magufuli hatunaye,
Kardinali analiaa, Magufuli hatunaye,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Bagonza na Munga, JPM mlimpenda,
Kilaini na Nyaisonga, JPM limpenda,
Mwingira na Shoo, JPM mlimpenda,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Kitima omboleza, Ruwaichi omboleza,
Niwemugizi alia, Masheikh omboleza,
Upendo mlimpa, BWANA atawalipa,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Babangu Hezbon, Doris mamangu,
Swali wananiuliza, nini mwanangu?
Magufuli amekufa, uuuwiii Mungu!
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Kaushwe mwili, zikwe kaburi la wazi,
Makumbusho jama, jengee Magufuli,
Kijijini kwao Mlimani, Chato wilayani,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Enzi zako Magufuli, FFU ilipumzika,
Enzi zako Magufuli, chinga pumzika,
Enzi zako Magufuli, mamantilie tulia,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Majambazi likizoni, wakati wako JPM,
Mavibaka likizoni, wakati wako JPM,
Mafoleni likizoni, wakati wako JPM,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Umeme bwerere, wakati wako Pombe,
Maji pia bwerere, wakati wako Pombe,
Mitandao huree, wakati wako Pombe,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
King’ongo ulijenga, ndani ya siku sita,
Chini ya mti wasoma, mtandaoni liona,
Ulitoa amri siku saba, ukingali Kahama,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Shujaa wa Uviko, Magufuli ameenda,
Katuachia kiboko, rais Suluhu Samia,
Mbele pambano, muenzi JPM shujaa,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Magufuli ni Nabii, maono alipewa,
Corona iko njiani, ukaliandae taifa,
Weka huduma za jamii, lipone taifa,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Usifunge mipaka, JPM aliambiwa,
Mataifa yatakuijia, wapate kupona,
Usizuie ndani wana, Tz inaponywa,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Kama Yohana Mbatizaji, JPM likuja,
Kumsafishia mahali, Suluhu Samia,
Njiani watu wengi, ka nzige jani wala,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Bilioni tatu unusu, ni nusu ya dunia,
Asema waziri mkuu, wamombolezea,
Amini msiba huu, JPM rekodi avunja,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Marais kumi na saba, JPM wamezika,
Hawakuijali Corona, inayotesa dunia,
Wamejali tu mahaba, JPM aliyowapa,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Jamani Janet ataliaje, albino wataliaje,
Suzi mamake ataliaje, watoto walieje,
Elimu bure taliaje, watekamaji taliaje,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Wastaafu wataliaje, wakulima walieje,
Wavuvi wataliaje, wafugaji wataliaje,
Wajawazito wataliaje, elimu ya juu je?
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Macho mekundu pia, uuaji meondoa,
Wafugaji na wakulima, vita meondoa,
Za utotoni mimba, vita umeimarisha,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Pombe njaa ulifuta, ujambazi ulifuta,
JPM wavivu ulifuta, wapigaji ulifuta,
Kibiti ugaidi futa, ukajenga viwanda,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Viongozi wenzio, marais waliostaafu,
Wapunga upepo, hawana usumbufu,
Uliwaenzi wenzio, atakulipa Mungu,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Majini tuko vizuri, angani tuko vizuri,
Umeachia nchi meli, nchi yote eapoti,
3500 km za lami, zafika Oman nchini,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Treni nchi nzima, ya wese mabomba,
TBC nchi nzima, umeme nchi nzima,
Afya nchi nzima, shule umetapakaza,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Rada nchi nzima, Burundi na Rwanda,
Zao ndege zaongozwa, toka Tanzania,
JPM alama umeacha, ndani kimataifa,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Sadaka ulikusanya, uchafu likusanya,
Michango ulikusanya, kodi likusanya,
Mabandani ulikula, ubugobugo lipiga,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Mikutano ulivamia, pasina kualikwa,
Ulibadili mijadala, lilenga kupata tija
Maslahi ya umma, mbele litanguliza,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Burundi lipatanisha, Sudan patanisha,
DRC ulipatanisha, Kenya lipatanisha,
Rwanda lipatanisha, Zenji lipatanisha,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Malawi tegemea meli, DR Congo pia,
Burundi tegemea meli, nayo Zambia,
Kisumu tegemea meli, nayo Uganda,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Comoro tegemea, ndege za Tanzania,
Maziwa Makuu pia, bandari tegemea,
Sehemu ya Afrika, hospitali tegemea,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Kinematics potea, Pythagoras potea,
Logarithms potea, Quadratics potea,
Kemikali potea, Quantitatives potea,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Wasomi uliteua, hukutumbua pasaka,
Misikiti ulijenga, BAKWATA swalia,
Jemedari nenda, Amiri Jeshi tangulia,
Komando nenda, Kamanda tangulia,
WAPO kazike Chato, FGBFC kazike,
AGAPE kazike Chato, EAGT kazike,
TAG kazike Chato, GRC pia mkazike,
Magufuli alituhimiza, ibada tuishike.
Samia ambie wapigaji, ehiii baghosha,
Samia ambie mafisadi, ehiii baghosha,
Samia ambie walaghai, ehiii baghosha,
Samia ambie maghaidi, ehiii baghosha.
Tarehe kumi saba, JPM sikukuu yake,
Miaka ataenziwa, ka shujaa wengine,
Pombe shujaa, kongamano andaliwe,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Utamu wa Magufuli, ule wake ukali,
Utamu wa pilipili, ni ule wake ukali,
Wampenda wahisani, fedha lidhibiti,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
John hesabu peleka, mbele ya waasisi,
Wa yetu Tanzania, Nyerere na Abedi,
Aambie Tanzania, ni uchumi wa kati,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
JPM salimia Mandela, salimia Aristotle,
JPM salimia Plato pia, salimia Moringe,
Pombe Newton salimia, salimia Socrate,
Magufuli Marx salimia, salimia Nyerere.
John salimia Odinga, salimia pia Stalin,
John salimia Mao pia, na Chirwa Orton,
John sabahi Fidel pia, na Katabalo Stan,
JPM Gandhi salimia, Mkapa na Tubman.
JPM Sankara salimia, Olympio salimia,
JPM Nasser salimia, Anwar pia salimia,
JPM Luthuli salimia, Nkrumah salimia,
JPM Lenin salimia, Ceausescu salimia.
JPM habari pelekee, hao wote wajamaa,
Waambie dunia ile, sasa ni kijiji kimoja,
Eti Mabeberu wote, wakaa na Wajamaa,
Mabeberu wenyewe, ndiyo wanawekeza.
Misahafu ingekuwa, inaandikwa hii leo,
Magufuli ungekuwa, na maandiko yako,
Stalin pia aliijenga, Urusi miaka mitano,
Tubman pia aliijenga, Liberia hivohivyo.
Ulilala saa kumi, kwa ajili ya Tanzania,
Saa Kumi na mbili, Magufuli uliamka,
Ka yule Ujerumani, Bi Merkel Angela,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
University of Magufuli, Chato wekeni,
Kumuenzi jemedari, fundishe kozi hii,
Uongozi mkakati, na ubunifu mkakati,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Tulie kwa tumaini, sijemkwaza Mungu,
Tulie kwa tumaini, sijemkwaza Mungu,
Tulie kwa tumaini, sijemkwaza Mungu,
JPM utafufuliwa, katika kiama ya wafu.
Tanga ninaanua, tutaonana Paradiso,
Twonane Paradiso, twonane Paradiso,
Twonane Paradiso, penye mji wa raha,
JPM tafufuliwa, katika kiama ya wafu.
Jina kamili la Mtunzi ni: Douglas O. Majwala.
Jina la Ushairi ni: The Rod of Grace/Fimbo ya Musa.
majwalaoriko@yahoo.co.uk