Hili wazo halikuwa baya kama tulivyokuwa tumelichukulia. Vijana wengi wenye nguvu wakipata fursa za kujiunga na jeshi, wanaacha vipaji vyao kwenda huko. Wachache sana wanapata nafasi ya kuvitumikia wakiwa jeshini ila wengi majukumu yao hayawaruhusu kufanya hivyo kwa hiyo vinapotea.
Sekta za michezo zingekuwa zimesimama na kuwa uwezo wa kushindana kimaslahi kwa ajili ya vijana, nchi hii ingefaidika sana.