MAGUFULISM: Falsafa ya Magufuli kwenye Siasa, Uchumi N.k

Hizi ni sifa za mbowe
 
Mtoa uzi umesahau kuweka CV yako na namba ya simu mwishoni[emoji23][emoji23],au umechoka baada ya kuvizia teuzi na kukosa enzi za JPM[emoji134][emoji134]
 
Isome vizuri historia ya dunia ilipotoka na ilipofika, jitahidi pia kutembea na kujionea maendeleo ya dunia sehemu mbalimbali..

Mzee wetu hakuwa na jipya, aliwaza kizamani karne ya 21 na hapo ndio tatizo lilipoanzia na kutofutiana na watu.....Alikuwa anajaribu kulazimisha watu na dunia iishi anavyofikiri yeye akiamini ana akili nyingi sana kumbe wenzie wanamuona ana fikra za kizamani....
 
Umeandika kitu ambacho niliwahi kuandika hapa pia. Shujaa alikuwa na NIA NJEMA kabisa ya kutaka Tanzania ipige hatua mbele, ila tatizo hakuwa KIONGOZI mwenye MAONO na alipo pata MAONO hakuwa na namna nzuri ya kuyafikia maono yake.

Sehemu alivyo-fail Shujaa ni 'how to execute' mipango ili kutimiza maono! Aliamini katika 'YEYE' kuliko katika 'SISI', aliona wengine wote hawana uwezo wa kutimiza mambo isipokuwa yeye tu na ndiyo maana alikuwa mtoa AMRI wa kufanyika jambo siyo mtu wa MSHAURIANO.

Shujaa alipaswa kuwa MTEKELEZAJI wa maelekezo ya KIONGOZI siyo MTOA MAELEKEZO ya kutekeleza.
 
Magufulism ni falsafa inayoamini kuminya vyombo vya habari,vyama vya siasa na asasi za kiraia ikiamini kufanya hayo ni kushinda uchaguzi.

Inapojikuta ni total mess n failure Magufulism inabadilika sasa na kuelekeza wizi wa kura wazi wazi.
 
Tuombe sana huko mbele asitokee wa kuturudisha nyuma kama alivyofanya huyu.
 
Magufuli na Elimu...
Magufuli na Afya...hapa amejenga Vituo vya huduma za afya zaidi ya 400
Hospitali ya Uhuru
Kujenga vituo vya afya 400 bila kupeleka dawa na wataalamu ni matumizi mabaya ya fedha.
 
Mtazidi kuweweseka sana
 
Pole sana maana kwa sasa tupo na mama yetu Samia.
 
Mkuu mi naunga hoja kwa kishindo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…