Mahaka Kuu yakataa kutoa amri ya kusitisha maandamano

Mahaka Kuu yakataa kutoa amri ya kusitisha maandamano

jiamini360

Member
Joined
Jan 26, 2016
Posts
35
Reaction score
19
Mzozo kuhusu tume inayosimamia uchaguzi nchini Kenya IEBC umeendelea kutokota. Waandamanaji katika miji mbalimbali wameendeleza maandamano yao ya kila Jumatatu kushinikiza tume hiyo ivunjwe na iundwe upya, kama upinzani unavyosisitiza.

Mapema Jumatatu mahakama kuu ya Nairobi ilikataa kupiga marufuku maandamano hayo yanayoongozwa na muungano wa upinzani CORD. Mahakama hiyo ilisema maandamano yanakubalika kisheria na ni wajibu wa polisi kuhakikisha kuwa yanafanyika kwa amani. Baadhi ya wabunge wa chama kinachotawala Jubilee walitaka mahakama kuharamisha maandamano hayo.

Kisumu mtu mmoja amepigwa risasi na kukimbizwa katika hospitali. waandamanaji wamechoma matairi kwenye barabara hali ambayo imetatiza shughuli za usafiri.Ghasia zimeendelea katika mji huo licha ya mkuu wa polisi kuwaonya watu na kuwataka wazishiriki maandamano hayo.

Katika jiji kuu la Nairobi waandamanaji wamejitokeza wakilenga kufika katika ofisi za tume ya IEBC zilizoko katikati ya mji huo.

chanzo:bbcswahili na dw
 
Nimewapenda hao MAJAJI wamesimamia sheria.Sasa Polisi ndiyo wajiulize walipokosea
 
Back
Top Bottom