1. Jambo haliwezi kuwa subjudice kama haliko mahakamani tayari. Hivyo kwenda mahakamani ili kulifanya jambo linalojadiliwa liwe subjudice ni kinyume na maana na makusudi ya convention yenyewe
2. Mahakama haina mamlaka Si kisheria wala Kwa convention au precedent kuliamrisha Bunge lisijadili jambo lolote. Hivyo kama wameandika barua hiyo ni muhimu kwa Bunge kufungua shauri la kuwa-impeach majaji waliotoa amri hiyo batili.
3. Bunge ni wawakilishi wa wananchi.. Wanananchi ndio wenye mamlaka Ya mwisho ndani Ya nchi na ndio msingi wa immunity ya Bunge. Kwamba wananchi wako huru kujadili jambo lolote, wakati wowote ikiwa ni pamoja na mahakama yenyewe. Na uhuru huo wanajipa wenyewe maana ndio wenye nchi.
4. Mfano Nchini UK kulikuwa na amri Ya mahakama(Super Injunction order) Kuwa watu Fulani maarufu wasitajwe kuhusika na mchepuko (extra marital affairs) kitendo hiki kiliwaudhi wabunge wakaamua kuwajadili na kuwataja majina bungeni hivyo zile amri zikabidi zifutwe maana zilipoteza maana.