Mahakama Kenya yaamrisha Miguna Miguna kurudishwa nchini

Mahakama Kenya yaamrisha Miguna Miguna kurudishwa nchini

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
3EA15111-562D-425C-BDF1-0BB2AA0061C6_w1023_r1_s.jpg

Mahakama Kuu nchini Kenya Jumatatu imetoa amri kwa maafisa wa Uhamiaji nchini humo kumruhusu mwanachama wa upinzani kurejea nchini baada ya kuondolewa kwa nguvu mapema mwezi Januari 2018.

Jaji wa mahakama hiyo Chacha Mwita ameiamuru idara ya Uhamiaji kumpa Miguna hati zake za kusafiria ili kumwezesha kurudi nchini Kenya mpaka hapo shauri lake litakaposikilizwa mahakamani juu ya uhalali wa uraia wake.

Miguna Miguna ambaye ni mwanachama wa Muungano wa upinzani Nasa na pia ni wakili alilazimishwa kupanda ndege na kurudishwa nchini Canada.

Kufukuzwa huko nchini kulifuatia kukamatwa kwake na kufunguliwa mashtaka ya uhaini kwa kuhusika na zoezi la kujiapisha kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Odinga ambaye ameendelea kusisitiza kuwa ndiye mshindi halali wa uchaguzi mkuu wa urais nchini Kenya uliofanyika mwaka 2017.

Wizara ya Mambo ya Ndani ilieleza kuwa Miguna alikana uraia wake wa Kenya baada ya kuchukua ule wa Canada miaka kadhaa iliyopita.

Chanzo: VoA
 
Hio report ni ya kitambo sana na migration department walishamjibu huyo judge uchwara. no something new.
 
Aisee kwanini katiba yetu isiwe na nguvu hivi

Mungu ni Pendo
 
Unajua walimpeleka na ndala anafuata viatu ila si ana Passport ya Canada aombe Visa on arrival ha ha ha
 
Lengo la Miguna2 nini haswa...mbona simuelewi...Huyu si ndiye akiyeandika vitabu vya dhihaka dhidi ya Raila? If I was Raila I would never trust him... Lengo lake labda ni umaarufu tu anatafuta kisiasa..However his right of citizenship should not be revoked...
 
Hio report ni ya kitambo sana na migration department walishamjibu huyo judge uchwara. no something new.
They have eyes lakini hawayatumii kusoma.......uchwara kwa sababu hakusema kama ulivyotaka......

Court orders Matiang'i, Kihalangwa to facilitate Miguna's return
Feb. 26, 2018, 12:00 pm
By CAROLE MAINA and NANCY AGUTU @thestarkenya

1709551_5.jpg

The High Court has ordered Immigration boss Gordon Kihalangwa to issue lawyer Miguna Miguna with his travel documents to enable his return forthwith.

Judge Chacha Mwita said that failure to comply with the directive, the self-declared NRMKe General is at liberty to use his Canadian passport to return to Kenya.

"Issue him with the travel documents and he should be allowed to Kenya on a day he chooses and to remain within the country until his petition his heard and determined," he said.

"The orders should be served in the Standard and the Nation Newspapers," the judge said.
 
Unajua walimpeleka na ndala anafuata viatu ila si ana Passport ya Canada aombe Visa on arrival ha ha ha

si uchukua dakita tau usome uelewe ruling ya leo...
kipande kidogo hapa

Back
Top Bottom