Mahakama kuamua kesi ya Kinana leo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.PICHA|MAKTABA


KWA UFUPI
Ni kesi ya Abdulrahman Kinana kumtaka Peter Msigwa kufuta kauli yake.


Dar es Salaam. Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, leo inatarajiwa kutoa uamuzi, dhidi pingamizi zilizowasilishwa na upande wa mlalamikiwa kwa njia ya maandishi dhidi ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Kinana anamtaka Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, kufuta matamshi ya kumkashifu, kumfedhehesha na kumhusisha na ujangili wa meno ya tembo.

Uamuzi huo, unatarajiwa kutolewa na Jaji Zainabu Muruke, baada ya Mchungaji Msigwa kupitia wakili wake, Peter Kibatala kuwasilisha kwa njia ya maandishi, pingamizi lake dhidi ya mlalamikaji ambapo anaiomba mahakama hiyo kuifuta kesi hiyo kwa madai kuwa ina upungufu kisheria.

Kwa mujibu wa Msigwa kupitia wakili wake Kibatala wanadai kuwa kesi hiyo iliyofunguliwa na Kinana dhidi yake, haina mashiko kwa sababu ilikosewa jinsi ya kufunguliwa.

Walidai kuwa kesi hiyo ilikosewa namna ilivyofunguliwa Ilipaswa kufunguliwa mkoani Mwanza ambapo tukio linadaiwa kutokea ama mkoani Iringa kwenye makazi ya kudumu ya Mchungaji Msigwa. Hivyo wanaiomba mahakama kuifuta kwa sababu ina upungufu wa kisheria.

Kinana anaiomba mahakama iamuru Mchugaji Msigwa amlipe kiasi cha Sh 350 milioni kutokana na matamshi ya Aprili 21, 2013, yaliyotolewa katika mkutano wa hadhara.chanzo. http://www.mwananchi.co.tz/habari/K...a-leo/-/1597296/2146402/-/jo3uxa/-/index.html



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…