Mahakama kutoa uamuzi kuhusu kesi dhidi ya Kaimu IGP wa Kenya wiki ijayo

Mahakama kutoa uamuzi kuhusu kesi dhidi ya Kaimu IGP wa Kenya wiki ijayo

Ikaria

Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
93
Reaction score
238
Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli anatarajiwa kuhukumiwa kifungo Ijumaa ijayo kwa kosa la kupuuza maagizo ya Mahakama mara saba.

Jaji Lawrence Mugambi ameeleza kuwa IGP amedharau mahakama kwa kukosa kufika mbele yake mara 7 kueleza kuhusu maisha ya Wakenya watatu wanaodaiwa kutekwa mjini Kitengela Agosti 19, 2024 na hadi sasa hawajulikani waliko.

IGP alikosoa kufika mahakamani kueleza waliko mwanaharakati Bob Micheni Njagi na ndugu wawili Jamil Longton na Nadim Hamed, wote wanaodaiwa kutekwa na watu wanaoaminika kuwa ni polisi wakitumia gari aina ya Subaru.

Visa vya utekaji vimeonekana kukithiri tangu alipochukua madaraka Rais Ruto na hasa tangu kuzuka kwa vuguvugu la maandamano ya GenZ.
GWuk1EeWIAAcye0.jpg
 
Back
Top Bottom