Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 673
- 1,318
Moja ya kesi muhimu katika uhuru wa kimtandao Tanzania ni pamoja na hii, Bwn. Paul Kisabo aliwasilisha malalamiko dhidi ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kisabo alidai kuwa TCRA imezuia ufikiaji wa mtandao maarufu wa kijamii wa mijadala ya sauti, Clubhouse, hatua aliyodai kuwa inakiuka haki zake za kikatiba na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeiridhia.
Kisabo alieleza kuwa Clubhouse ni muhimu kwake kwa mawasiliano na kupata taarifa za kitaifa na kimataifa. Alisema kuwa kuzuia ufikiaji wa jukwaa hili na kumlazimu kutumi VPN ni ukiukwaji wa haki zake za kikatiba zilizoainishwa katika Ibara za 18(1)&(2), 20(1), 26(1) na 29(1)&(5) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na mikataba mbalimbali ya kimataifa kama Azimio la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu (UDHR), Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR), na Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu (ACHPR).
Kisabo aliomba mahakama itoe amri zifuatazo:
Kisabo aliomba mahakama itoe amri zifuatazo:
- Kutangaza kuwa zuio hilo linakiuka Katiba ya Tanzania pamoja na mikataba ya kimataifa.
- Kutangaza kuwa yeye na Watanzania wengine wana haki za kikatiba pamoja na za kimataifa za kufikia na kutumia mtandao wa Clubhouse bila vizuizi.
- Amri za muda kuwa waruhusiwe kufikia na kutumia Clubhouse wakati kesi inaendelea bila vizuwizi.
- Amri kuwa waruhusiwe kufikia na kutumia Clubhouse bila vizuizi baada ya hukumu kutolewa.
Upande wa serikali ambao wao ndio walikua walalamikiwa walikanusha madai hayo, wakidai kuwa hawajazuia ufikiaji wa Clubhouse na kwamba hawawezi kuthibitisha kama Clubhouse imezuiwa kwa sababu hawamiliki mtandao huo.
Kwakua kesi hii ni ya kikatiba, mahakama kuu ilikaliwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Mh. U.J Agatho akiwa pamoja na Mh. F.K Manyanda pamoja na Mh. A.K Rumisha waliamua yafuatayo;
Kwakua kesi hii ni ya kikatiba, mahakama kuu ilikaliwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Mh. U.J Agatho akiwa pamoja na Mh. F.K Manyanda pamoja na Mh. A.K Rumisha waliamua yafuatayo;
- Mahakama ilikubaliana kuwa Kisabo na watanzania wote wana haki ya kikatiba ya kupata huduma ya Clubhouse katika ibara za 18,20,26 na 29 za katiba, lakini haki hiyo ina mipaka inayotakiwa kufuatwa kulingana na ibara ya 30(2) ya Katiba
- Mahakama ilibaini kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa kulikuwa na vizuizi vya upatikanaji wa huduma ya Clubhouse nchini Tanzania.
- Ombi la Kufungua Upatikanaji wa Clubhous lilikataliwa kwa sababu hakukuwa na ushahidi wa kuwepo kwa vizuizi hivyo. Mahakama ilieleza kuwa upatikanaji wa huduma ya Clubhouse unaweza kuwa na mipaka halali na ya kisheria ikiwa kuna sababu za msingi.
- Gharama za Kesi:Mahakama iliamuru kila upande kubeba gharama zake wenyewe kwani kesi hii ilikuwa ya kikatiba.
Kwa ujumla, mahakama ilikubaliana na baadhi ya madai ya Kisabo lakini ilikataa mengine kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha wa kuwepo kwa vizuizi vya upatikanaji wa mtandao wa Clubhouse.
Sijajua ni ushaidi wa namna gani Mahakama inauhitaji🤔, lakini binafsi nina zaidi ya mwaka siupati mtandao wa Clubhouse kabisa, au kuna wanao upata (bila VPN) ❓. Anyway, Kongole Bwn. Kisabo 👏, umewakilisha sauti za wengi.
Pia soma Mahakama Kuu yadai hakuna ushahidi wa Serikali kufungia Mtandao wa Clubhouse
Sijajua ni ushaidi wa namna gani Mahakama inauhitaji🤔, lakini binafsi nina zaidi ya mwaka siupati mtandao wa Clubhouse kabisa, au kuna wanao upata (bila VPN) ❓. Anyway, Kongole Bwn. Kisabo 👏, umewakilisha sauti za wengi.
Pia soma Mahakama Kuu yadai hakuna ushahidi wa Serikali kufungia Mtandao wa Clubhouse