LGE2024 Mahakama Kuu Kanda ya Songea yatoa mafunzo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mahakimu wa Mkoa wa Ruvuma

LGE2024 Mahakama Kuu Kanda ya Songea yatoa mafunzo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mahakimu wa Mkoa wa Ruvuma

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Mahakama Kuu Kanda ya Songea imetoa mafunzo ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa waheshimiwa mahakimu wakazi kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma.

Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Huntlcub Ruhuwiko mjini Songea,yamefunguliwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea Mheshimiwa James Karayemaha.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo,Jaji Mheshimiwa Karayemaha amesema Mahakama hiyo iliandaa sera ya mafunzo ya mwaka 2019 kwa lengo la kushusha mafunzo kwenye Kanda hiyo.

Amesema mafunzo hayo yameandaliwa kama sehemu ya utekelezaji wa sera hiyo ambayo yatawajengea uwezo waheshimiwa mahakimu kufahamu sheria mbalimbali zinazohusiana na uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa kwa mwaka 2024.

Soma Pia:
“Mafunzo ya uchaguzi wa serikali za mitaa ,yatawasaidia kujua sheria,kanuni na taratibu zinazoongoza uchaguzi,yatasaidia kujua namna bora ya kupokea ,kusikiliza na kuamua migogoro ya aina yoyote itakayoletwa mbele ya mahakimu’’,alisisitiza.

Hata hivyo ameutaja uchaguzi wa serikali za mitaa ni suala muhimu katika ustawi wa demokrasia nchini ambapo waheshimiwa mahakimu wote wa Tanzania ni sehemu ya mchakato wa kufanikisha uchaguzi wa serikali za mitaa ambao ni makamishina wa viapo.

Amewataja waheshimiwa mahakimu kuwa ndiyo watakaowaapisha wasimamizi wa uchaguzi na viongozi watakaochaguliwa kabla ya kuanza rasmi kufanya shughuli zao kwa mujibu wa sheria.

Katika hatua nyingine Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea amewahimiza watumishi wa Mahakamu kufanya kazi kwa kusikiliza na kutoa maamuzi kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA hivyo kuachana na matumizi ya karatasi.

Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo hayo Hakimu Mkazi Mfawidhi,Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Songea Mheshimiwa Japhet Manyama amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa waheshimiwa mahakimu kwa lengo la kuwaandaa kwa ajili ya kusikiliza na kuamua mashauri yatakayotokea wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Amelitaja lengo kuu la mafunzo hayo kuwa ni kuwaandaa na kuwapitisha mahakimu katika sheria zinazohusu uchaguzi zikiwemo kanuni zinazotumika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na kuwaandaa namna ya kumudu msukumo wa kisiasa na jamii kwa kuangalia sheria ili waweze kutoa maamuzi ya haki kwa wote.
 
CHADEMA HAWATAKI VIJANA WAJIANDIKISHE, JE WANAWAOGOPA KWENYE UCHAGUZI?

Sauti za Chadema sasa zinapaza malalamiko yasiyo na mashiko, wakidai kwamba Tume ya Uchaguzi (NEC) inaandikisha wanafunzi kwa lengo la kuwaandaa kupigia kura CCM. Ukweli ni kwamba, kila kijana mwenye miaka 18 ana haki ya kikatiba kujiandikisha na kupiga kura.

Hii siyo mbinu ya kisiasa bali ni utekelezaji wa sheria, kwani vijana waliozaliwa mwaka 2006, wakiwemo wa umri wa miaka 17 mwaka huu, watafikisha miaka 18 ifikapo mwakani. Je, Chadema wanataka kuwanyima haki zao kikatiba?

Chadema wanatakiwa kuelewa kuwa kila aliyeandikishwa ameonesha kitambulisho kinachoonesha umri wake halali. Kuibua tuhuma za "kuandikisha watoto" bila kutoa ushahidi wa vitambulisho ni mbinu ya kisiasa ya kutengeneza mazingira ya kujiondoa mapema au kutafuta kisingizio endapo watashindwa tena mwakani. Tumeona mbinu kama hizi mara kadhaa—wakishindwa, hukimbilia kusema "tulibambikiwa."

Nani anaweza kuwazuia vijana wenye ari na shauku ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi? Hili si swali la wafuasi wa CCM bali ni ishara ya hofu ndani ya Chadema, wakijua kuwa kizazi cha sasa kinatambua haki zake na hakitadanganywa kirahisi. Wanapojaribu kupinga ushiriki wa vijana, wanaonesha wazi kuwa hawataki sauti za kizazi kipya zisikike.

Kwa kifupi, malalamiko ya Chadema si hoja ya msingi bali mbinu ya kuwatisha vijana na kuwapotezea imani katika mchakato wa uchaguzi. Uchaguzi si mchezo wa kuigiza bali ni nafasi ya kila raia, awe kijana au mzee, kuamua hatma ya taifa kupitia sanduku la kura.

Kama Chadema wana hofu ya kushindwa, basi wanapaswa kujipanga na kuja na sera bora badala ya kutengeneza visingizio visivyo na msingi.
 
Back
Top Bottom