Mahakama Kuu (?) Ya Dar

Ninux

Member
Joined
Oct 9, 2016
Posts
34
Reaction score
10
Hamjambo, samahani kwa urefu!
Mzanzibari alinidanganya na sasa anajaribu kuniibia mali yangu!
Kwa hiyo nilinunua kiwanja kule Unguja lakini wote, hasa Sheha wa Michamvi, Abeid J. Haji, waliniambia nitumie jina la mzanzibari, Suzan A. Mrope S. A. M.)
Mwanzoni nilikuwa na wasiwasi kwa sababu nilijua kwamba wazungu wengi wameshatapeliwa, lakini nilichanganywa na Sheha, niliyemfikiri anajua vizuri sheria.
Basi nilikubali lakini nilitaka huyu S.A.M. ale kiapo rasmi kwa maandiko mbele ya mwanasheria na mashahidi. Alifanya hivi na mimi nilisajili rasmi kiapo chake.
Basi baadaye nilihisi kwamba walikuwa wanapanga utapeli kwa hiyo nilikwenda Idara ya Ardhi na niliwaandikia malalamiko nikawaeleza kila kitu na niliambatisha kiapo cha S. A. M.
Mwenyekiti wa Bodi alifanya upelelezi. Alikubali kwamba S.A.M. alinidanganya kwa sababu pamoja na sheha walificha kwamba ninaruhusiwa kupata "lease". Kwa hiyo alifuta cheti S.A.M. alichopata na nilipata "lease" kwa jina langu.
Kwa bahati mbaya S.A.M. alikataa kurudisha cheti kilichofutwa na alifungua kesi ya madai!
Wakati wa usikilizaji S.A.M. alishindwa kutoa ushahidi kwamba yeye alinunua kiwanja.
Mimi nilitoa ushahidi na wote walikubali kwamba kweli nilinunua kiwanja.
Uamuzi wa Jaji, Said H. Khalfan, ulinishangaza sana.
Alisema kwamba barua ya Bodi ya Ardhi inakosea kifungu cha sheria kwa hiyo mmiliki halali ni S.A.M.! Wakati wa usikilizaji jaji alificha hitilafu hiyo ingawa wamehojwa mashahidi kutoka Idara ya ardhi. Jaji hakujali kabisa kiapo rasmi cha S.AM.

Lakini katika "judgement", yaani sababu ya uamuzi, aliandika hivi:
"To cut the story in this the plantiff [S.A.M] is the rightful owner of the disputed area unless otherwise the Land Transfer Board follow the proper provision for revocation as stipulated under section 18B of Land Transfer Act no. 8/1994 (regulations to amend tge land Transfer regulations at 2011 available under legal note no. 88"!

Wakili wangu, bi. Salma (Apex Attorneys, Culture Building, Vuga) alikata rufaa bila kushughulia marekebisho ya barua ya Bodi ya Ardhi.
Mimi nilifaulu kupata marekebisho lakini Mahakama Kuu walikata kupokea Barua mpya ya Bodi na walikataa rufaa.

Sasa niliambiwa kwamba yule bi.Salma (mwenye kujivuna sana) alifanya kosa kubwa alipokata rufaa.

Mwenyekiti wa Bodi, Mwenyekiti wa Mahakama ya Ardhi na mawakili wote waliniambia nisiwe na wasiwasi kwa sababu barua mpya ya Bodi pamoja ya "lease" zinaonyesha wazi kwamba mmiliki wa kiwanja.
Huyu mwizi, S.A.M., alirudi mahakamani akaimba amri ya utekelezaji wa uamuzi... akapata.

Wakili wangu mwengine anataka kukataa rufaa kwenye mahakama ya Dar.
Mimi nina wasiwasi.

JE, ATARUHUSIWA KUTOA BARUA MPYA YA BODI KAMA USHAHIDI MPYA?
TAFADHALI ANAYETAKA KUNIAMBIA NIKUTANE NA MWANASHERIA AJUE KWAMBA MIMI SI MJINGA. ASANTE.

Huku Zanzibar mawakili wana kiburi sana na wanajivuna; haiwezekani kujadiliana nao. Wote wanafikiri kwa wateja ni wajinga!

Ninawashukuru wote wanaonisaidia.

Wengine wajue kwamba si lazima kujibu.
 
Msingi wa kesi upo kwenye kudanganywa kutumia jina la S.A.M.

sio rahisi udanganye jina halafu ubaki salama.
 
Kama bodi ya ardhi inakutambua wewe ukengeufu wa jaji hautaipoteza haki yako.

Ngangamala.
 
Kesi unashinda mapema!
Ila ikija bara,kwa huko watakukamuaaa
 
Msingi wa kesi upo kwenye kudanganywa kutumia jina la S.A.M.

sio rahisi udanganye jina halafu ubaki salama.
NInakushukuru kwa msaada wako. NItafuata ushauri mzuri wako.!
 
Tafuta wakili bara halafu uje nae huku znz afanye kufuatilia.
Kesi itaisha mda mfupi sana na utapata haki yako!
Waoga mno akiwatokea mtu anaye jiamini.
Piga mkwala heavy..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…