Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam leo tarehe 14, Februari 2025 imetupilia mbali shauri la kikatiba lililofunguliwa na Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga Mpina juu ya kupinga uaagizwaji wa sukari nje ya nchi.
Uamuzi wa shauri hilo umesomwa na Jaji Salma Maghimbi akieleza kulifuta huku akisistiza kuwa mahakama haijaona athari kwa wakulima wa ndani bali ni uoga tu. Hata hivyo ameeleza kuwa wakulima hao wana nafasi ya kukata rufaa kama hawajaridhika na hukumu hiyo.
Soma Pia: Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya
Kwa upande wake mwakilishi wa wakulima wa miwa kutoka Kilombero, George Mzigowande amesema hawajaridhishwa na hukumu hiyo hivyo watakata rufaa katika Mahakama ya Rufani.