Mahakama Kuu yamwachia huru George Sanga na Wenzake wawili, Kada wa CHADEMA walishikiliwa kwa miaka 5 gerezani kwa tuhuma za mauaji

Mahakama Kuu yamwachia huru George Sanga na Wenzake wawili, Kada wa CHADEMA walishikiliwa kwa miaka 5 gerezani kwa tuhuma za mauaji

Rula ya Mafisadi

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2024
Posts
404
Reaction score
852
BREAKING NEWS NJOMBE.

George Sanga na Wenzake wawili waliokuwa wanatuhumiwa kwa kesi ya mauaji wamechiwa huru na Mahakama.

Mungu ametenda haki imeshinda

George sanga na wenza wameachiwa huru Mahakama Kuu - Njombe

Wakili Dickson Matata, Joseph Mbilinyi wazungumza
IMG-20241231-WA0061.jpg

Njombe. Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imewaachia huru makada watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa wameshitakiwa kwa tuhuma za mauaji ya kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Pia soma: Njombe: Viongozi wa CHADEMA pamoja na dalali wa mbao wakamatwa kwa kuhusishwa na mauaji ya Kada wa CCM Emmanuel Mlelwa

Makada walioachiliwa huru ni George Sanga, Gudluck Mfuse na Octatus Mkwela, ambao kwa pamoja walikuwa wakituhumiwa kwa mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kwa vyuo vikuu Mkoa wa Iringa, Emmanuel Mlelwa.

Katika kesi Na.52 ya mwaka 2024, washitakiwa hao walikuwa wakitumiwa kutenda kosa hilo walilodaiwa kulifanya mwaka 2020.

R4 za Mama Samia, matunda ya maridhiano hayo. Hongera na Samia na Mbowe. Lissu hakuwahi kwenda hata kumuona gerezani wala kumtetea mahakamani, Mbowe kapambana mpaka mwisho.

Lissu anahangaika na Mwanamapinduzi l, mtu wa hovyo kabisa asiye na historia Chadema.

Sasa atulie aache uchale na upashkuna wa kisiasa. Ajifunze siasa za kistaarabu, watanzania ni waelewa
 
Lazima aende, si kamtuma wakili wa chama?
Wewe mwongo mkibwa. Wakili wa chama, wakati watu tumechangishwa mara kadhaa kulipia gharama za mawakili!!

Msiwe mnaropoka vitu ambavho hamna uhakika navyo.
 
Wewe mwongo mkibwa. Wakili wa chama, wakati watu tumechangishwa mara kadhaa kulipia gharama za mawakili!!

Msiwe mnaropoka vitu ambavho hamna uhakika navyo.
Hata wewe umechanga? Risit please
 
BREAKING NEWS NJOMBE.

View attachment 3189318
George Sanga na Wenzake wawili waliokuwa wanatuhumiwa kwa kesi ya mauaji wamechiwa huru na Mahakama.

Mungu ametenda haki imeshinda
Nakumbuka Tundu Lissu alisema hawa ni kati ya Kesi tano zilizokuwa zimebaki.

Mungu ni Mwema sana.

Yule mzee kanda ya ziwa, tumemsamehe lakini hatutomsahau.
 
Anatoka anakuta wale aliyekuwa anawapigania wanaponda Raha na kugombia vyeo
 
  • Thanks
Reactions: UCD
R4 za Mama Samia, matunda ya maridhiano hayo. Hongera na Samia na Mbowe. Lissu hakuwahi kwenda hata kumuona gerezani wala kumtetea mahakamani, Mbowe kapambana mpaka mwisho.

Lissu anahangaika na Mwanamapinduzi l, mtu wa hovyo kabisa asiye na historia Chadema.

Sasa atulie aache uchale na upashkuna wa kisiasa. Ajifunze siasa za kistaarabu, watanzania ni waelewa
Ficha upumbavu wako kwenye mambo serious
Watu wameteseka miaka minne unaleta utumbo wako hapa
 
Back
Top Bottom