George Sanga na Wenzake wawili waliokuwa wanatuhumiwa kwa kesi ya mauaji wamechiwa huru na Mahakama.
Mungu ametenda haki imeshinda
George sanga na wenza wameachiwa huru Mahakama Kuu - Njombe
Wakili Dickson Matata, Joseph Mbilinyi wazungumza Njombe. Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imewaachia huru makada watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa wameshitakiwa kwa tuhuma za mauaji ya kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Makada walioachiliwa huru ni George Sanga, Gudluck Mfuse na Octatus Mkwela, ambao kwa pamoja walikuwa wakituhumiwa kwa mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kwa vyuo vikuu Mkoa wa Iringa, Emmanuel Mlelwa.
Katika kesi Na.52 ya mwaka 2024, washitakiwa hao walikuwa wakitumiwa kutenda kosa hilo walilodaiwa kulifanya mwaka 2020.
R4 za Mama Samia, matunda ya maridhiano hayo. Hongera na Samia na Mbowe. Lissu hakuwahi kwenda hata kumuona gerezani wala kumtetea mahakamani, Mbowe kapambana mpaka mwisho.
Lissu anahangaika na Mwanamapinduzi l, mtu wa hovyo kabisa asiye na historia Chadema.
Sasa atulie aache uchale na upashkuna wa kisiasa. Ajifunze siasa za kistaarabu, watanzania ni waelewa