Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam leo tarehe 14, Februari 2025 imetupilia mbali shauri la kikatiba lililofunguliwa na Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga Mpina juu ya kupinga uaagizwaji wa sukari nje ya nchi.
Uamuzi wa shauri hilo umesomwa na Jaji Salma Maghimbi akieleza kulifuta huku akisistiza kuwa mahakama haijaona athari kwa wakulima wa ndani bali ni uoga tu. Hata hivyo ameeleza kuwa wakulima hao wana nafasi ya kukata rufaa kama hawajaridhika na hukumu hiyo.
Kwa upande wake mwakilishi wa wakulima wa miwa kutoka Kilombero, George Mzigowande amesema hawajaridhishwa na hukumu hiyo hivyo watakata rufaa katika Mahakama ya Rufani.

Ikumbukwe Mpina, alifungua kesi ya kikatiba dhidi ya Waziri wa Kilimo, Waziri wa Fedha, Bodi ya Sukari, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na kampuni binafsi, akipinga uhalali wa utoaji wa vibali vya kuagiza sukari kutoka nje ya nchi. Mpina anadai kuwa vibali hivyo vilitolewa kinyume na sheria na taratibu zilizopo.
Katika hatua za awali za kesi hiyo, Mahakama Kuu ilitupilia mbali ombi la Mpina la kutaka kuwasilisha majibu ya nyongeza baada ya kupokea majibu kutoka kwa upande wa walalamikiwa. Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Arnold Kirekiano mnamo Septemba 18, 2024
Hata hivyo hadi sasa Mahakama Kuu ya Tanzania imeshindwa kutoa nakala ya Hukumu ya Kesi ya Wakulima wa Miwa wa Kilombero kupitia mtandao wa Mahakama uitwao Tanzill jambo linaloibua maswali mengi juu ya hukumu hiyo.