Mahakama kuwatenganisha mme na mke kwa muda.

Mahakama kuwatenganisha mme na mke kwa muda.

Joined
Apr 10, 2012
Posts
33
Reaction score
2
Msaada wa kisheria: Endapo wanandoa wameoana kwa zaidi ya miaka mitano hawana mtoto.Na wamefunga ndoa ya kiserikali. Katika ndoa yao kukawa na mgogoro wa muda mrefu uliopelekea kufikishana mahakamani na kisha mahakama kuwatenganisha kwa muda usiojulikana. Na ndoa ikaonekana iko beyond repair. Je muda gani wanandoa wanaweza peana talaka baada ya kutenganishwa kwa muda. Na je sheria inasemaje endapo mmoja wa wanandoa hao ataamua kuoa ama kuolewa katika kipindi hicho.
 
separation sio talaka huwez kuoa utakuwa na ndoa batl na mmoja wenu aweza omba fidia ya ugon
 
Hapa naomba mwanasheria afafanue zaidi kutengana ni kupi kwa ufahamu wangu mdogo najua ya kuwa watu wakitengana kwa miaka miwili ndoa inakuwa imevunjika?kama wanandoa wametengana zaidi ya miaka 4 bila kuwa pamoja na wakafungua kesi mahakamani je kule kutengana kwao ni halali au mahakama itatoa tena utengano wa miaka miwili?na mahakama ikifanya ivo itakuwa inasiidia au ina ongeza muda ?
 
Kutengana ni pale mahakama inapoamua kuwa mume na mke wasikae pamoja kwa muda. Dhumuni ni kuwafanya wenza hao wajirudi na kupatana. Kutengana kunaweza kutokea kwa namna mbili: ya kwanza kwa amri ya mahakama. Aina ya pili ni kwa mume na mke kfanya makubaliano ya kutengana. Makubaliano hayo lazima yawe kimaandishi na lazima yaseme vitu muhimu kama matunzo ya mama na watoto (kama wapo).

Athari za kutengana ni kuwa ndoa ipo hai (haijavunjwa) kwa hiyo kama ni ndoa ya mke mmoja, mume haruhusiwi kuoa kwa wakati huo. Kama akifunga ndoa, ndoa hiyo itakuwa batili. Ikiwa baada ya kutenganishwa mume au mke anaona hawezi kupatana na mwenzake hapo anaweza kufungua kesi ya kudai talaka. Talaka huwa inatolewa na mahakama tu baada ya mume/mke kufungua kesi.
 
Back
Top Bottom