KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 8,589
- 16,936
Mahakama Malawi yaamuru Nabii Shepherd Bushiri na mkewe kurejeshwa Afrika Kusini
Mahakama Kuu nchini Malawi imetoa uamuzi leo wa kurejeshwa kwa Nabii na Mchungaji maarufu raia wa Malawi, Shepherd pamoja na Mary Bushiri nchini Afrika Kusini.
Uamuzi huo umepokelewa kwa furaha na Serikali ya Afrika Kusini, ambayo ilifungua kesi patika Mahakama hiyo kutaka mchungaji huyo kurejeshwa Afrika Kusini kujibu mashatka yanayomkabili.
Mnamo mwaka 2020, Nabii huyo tajiri, Shepherd na Mary Bushiri walifikishwa mahakamani Afrika Kusini kwa mashtaka mbalimbali ya uhalifu. Hata hivyo, baada ya kupewa dhamana wakisubiri kesi zao kusikilizwa, walikiuka masharti ya dhamana na kutoroka nchini humo katika mazingira yasiyojulikana. Hatimaye, walibainika kuwa walikimbilia nchini kwao Malawi.
Kufuatia hilo, Afrika Kusini iliwasilisha ombi rasmi la kurejeshwa kwao nchini humo ili wakabiliane na mashtaka dhidi yao, yakiwemo ya Ubakaji, ukiukaji wa masharti ya dhamana, uvunjaji wa Sheria mbalimbali ikiwemo ya fedha, benki , usafiri wa anga na sheria ya uhamiaji.
kwa mujibu wa tarifa ya serikali ya Afrika Kusine, uamuzi huu unathibitisha uhuru wa mahakama, ushirikiano wa kimataifa, na imani ya umma katika mifumo ya kisheria kati ya Afrika Kusini na Malawi.
Hatua hii ni mafanikio makubwa katika ushirikiano wa kimataifa wa kisheria, ikionyesha uimara wa mifumo ya mahakama na diplomasia kati ya mataifa haya mawili. Pia, uamuzi huu unasisitiza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria na unaimarisha dhana ya uwajibikaji, uwazi, na kuheshimu mifumo ya kisheria katika nchi zote mbili. Kesi hii imevutia umakini mkubwa kutoka kwa umma na vyombo vya habari, ikilenga masuala mapana ya ufisadi na uwajibikaji.
Inaelezwa Nabii huyo anatarajia kukata rufaa kupinga kupelekwa Afrika Kusini, huku Serikali ya Afrika Kusini imeweka wadi pia kwamba itapinga rufaa yao iwapo wanandoa hao wataamua kufanya hivyo.