Mahakama mnatuonea watanzania wa hali ya chini!

Mahakama mnatuonea watanzania wa hali ya chini!

Ubavu

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2012
Posts
2,790
Reaction score
3,263
Leo nilitembelea mahakama moja wapo hapa jijini dar es salaam kwa nia ya kutiliwa saini kopi za vyeti vyangu vya elimu.
Nilikaribishwa vizur tu pale mapokezi. Nilipoeleza shida yangu, nilishangaa kupewa utaratibu mpya wa kupatiwa huduma hii muhimu hasa kipindi hiki ambacho ajira zimefunguliwa pamoja na vijana wengi wanaojiandaa na zoezi la maombi ya mikopo huko HESLB.

Jamaa wa mapokezi alinielekeza kusoma kwenye mbao ya matangazo ambapo kuna maelekezo mapya ya kufata ili upatiwe huduma ya kutiliwa saini kopi ya vyeti vyako.

Ambapo unatakiwa kwenda kulipia bank shilingi 5000/= kwa kila saini kwenye cheti chako. Mfano kama utaenda na vyeti sita, basi unatakiwa kulipia jumla ya sh30000/= ambapo kila kimoja ni sh 5000/=.

Sasa chukulia mimi kijana niliyemaliza chuo mwaka jana ambapo bado sijapata ajira hata ya kujishikiza, unaniambia nilipie pesa hizo tena kwa ajili ya kutia saini tu kwenye vyeti tena hapo bado sijajua kama hiyo ajira yenyewe ntapata! HAMUONI KAMA MNATUONEA KWELI?!

Kijana wa kimasikini kama mimi ambaye nilisomeshwa kwa shida na bibi yangu nimekaa mwaka mzima bila ya ajira (usiniambie habari za kujiajiri wakati mikopo mnaibana kwa masharti magumu) mnataka niitoe wapi hiyo pesa..?!

Bora ya mimi.. Kuna wale vijana wanaoomba mikopo HESLB ambao ndo kwanza wanaanza kutoka katika safari yao ya maisha, unadhani wanatoa wapi pesa hiyo?!

Nilipo mdadisi kwa undani yule mtu wa mapokezi, akasema wamepewa maelekezo kutoka juu eti "wanatakiwa kukusanya kodi ili kuongeza mapato ya mahakama". Sasa kodi mkusanye kwa wenye nazo jamani na sio sisi watu wa hali ya chini..! Niliamua kwenda mahakamani maana najua mahakama ni serikali pia ambapo gharama zitakuwa chini kidogo, lakini naona kabisa kuwa hakuna utofauti kati ya serikali na wakili private..!

Ombi langu: Jaji mkuu (au yeyote mwenye mamlaka) atoe tozo hii ambayo inaweza kuwanyima fursa za kuajiliwa vijana wa kitanzania ambao ndio wengi huku mitaani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa wa mapokezi alinielekeza kusoma kwenye mbao ya matangazo ambapo kuna maelekezo mapya ya kufata ili upatiwe huduma ya kutiliwa saini kopi ya vyeti vyako.

Ambapo unatakiwa kwenda kulipia bank shilingi 5000/= kwa kila saini kwenye cheti chako. Mfano kama utaenda na vyeti sita, basi unatakiwa kulipia jumla ya sh30000/= ambapo kila kimoja ni sh 5000/=.

Sasa chukulia mimi kijana niliyemaliza chuo mwaka jana ambapo bado sijapata ajira hata ya kujishikiza, unaniambia nilipie pesa hizo tena kwa ajili ya kutia saini tu kwenye vyeti tena hapo bado sijajua kama hiyo ajira yenyewe ntapata! HAMUONI KAMA MNATUONEA KWELI?!

Sent using Jamii Forums mobile app
.

Mkuu, hiyo ndio serikali. Haiangalii umaskini wako, inaangalia utoaji wa huduma.
hapo awali hapakuwa na utaratibu wa kulipia benki kwa vitu vidogo kama hivi, ilikuwa unaonana na hakimu anakuhudumia tu, au karani pia anakuunganisha kwa hakimu. Kwa sasa kuna utaratibu umewekwa, na umewekwa makusudi ili kudhibiti mianya ya rushwa na kuengezea mapato serikali. Huu ni wa kulipia benki kwa huduma zote zinatotolewa na mahakama.
Mahakimu hawakuipenda hii ya kulipia benki hadi kwenye kudhibitisha nyaraka mbalimbali kama vile vyeti. Hii walijua haina maslahi kwao, lakini hawana namna, uamuzi ulishatolewa.
Hata hivyo wapo Mahakimu wengine wanafanyia hizi shughuli nje ya ofisi, au hata majumbani kwao. Ofsini anaweza akuhudumie, lakini kwa siri kama vile mnapeana rushwa
 
Back
Top Bottom