Mahakama na kesi za matusi

Mahakama na kesi za matusi

Rweye

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
17,057
Reaction score
7,611
Kinachoonekana mbali ya kuwemo na mambo kibao ambayo yanakatazwa katika sheria ya uchaguzi ya 2010 naona sasa suala la matusi ndo limeonekana liwe msingi wa kesi dhidi ya CDM,lakini tuulize hivi... Mbona hatuoni kesi za rushwa ijapokuwa ukweli ni kwamba takribani wabunge 70% wa CCM walipita kwa kutoa rushwa?

Ama rushwa imeondolewa katika sheria hile na si sehemu ya maadili ya uchaguzi tena?
Nasema hivi kwasababu ukiangalia orodha ya mashitaka kwenye kesi ya kupinga ushindi Ubungo tayari kuna kipengele kinachodai JJ alimtukana Nghumbi

Ndugu zetu NEC,kipengele cha rushwa mmekitoa ama mnataka tuamini sheria hili ni ya matusi tu?
 
Mimi si mtalaam wa sheria, naamini judge kapotoka katika hukumu hii,kama kweli msingi wa kutenguwa ubunge umetokana na lugha aziitazo za matusi, sina hakika na hayo matusi husika yaliwezaje kushawishi binadam wenye akili timamu wakawahi asubuhi kwenye vituo vya kupiga kura na kumchangua mtoa matusi,labda kama hayo matusi yana msaada muhimu katika maisha ya kila siku ya wanachi wa jimbo husika.
Ningependa sana kama Lema angekata rufaa si kwa kutaka kuendelea na ubunge bali kuondoa hiyo precedence mbovu iliyowekwa na judge kwenye mfumo wa sheria zetu.
Inawezekana kabisa kwamba kuna lugha mabazo kwa mtazamo wa judge zilikuwa ni za matusi,lakini ni ajabu sana kuhusianisha ushindi wa mbunge na lugha za matusi.
Je,judge amepitia mikutano ya wote walioshiriki uchaguzi huo na kujiridhisha kuwa lugha ya namna hiyo ilitoka kwa mgombea wa CDM pekee ?
Inasemekana majaji hawakosei,nafikiri wao wanachemsha tu,hapa jaji kachemsha sana.
 
Back
Top Bottom