Mahakama ya kadhi hasa ni nini?

Mahakama ya kadhi hasa ni nini?

Raelish

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2013
Posts
489
Reaction score
162
Habarini ndugu zangu waislamu
Nawapenda kwa kuwa wote tumewekwa hapa duniani na Mungu mmoja,maana kuna Mungu mmoja tu mwenye uwezo wa kuumba binadamu. Kule jukwaa la siasa nimeona kuna maada inasema kuhusu uwepo wa mahakama ya kadhi kwenye katiba,wengi wamecomment walivyoona lakn mimi nina maswali kuhusu hii mahakama ya kadhi ili niielewe ndipo nijue nachangia nini.

Kwanza, naomba kujua mahakama ya kazi ni nini? pili,je ina umuhimu gani wa lazima kwa muislamu,je ni dhambi kwa muislam kuishi bila mahakama hii? Tatu,je ni sahihi na kuna umuhimu wowt wa kuingizwa kwenye katiba ambayo itatumika na watanzania wote,wenye dini na wasiokuwa na dini? Nne,je mahakama hii itawahukumu waislamu peke yao,na kama hivyo waislamu hawataruhusiwa kuhukumiwa kwenye mahakama zingine(za kawaida)? Mwisho,wale wasio waislamu haitawahusu kwa namna yoyote ile?

Tafadhali ustaarabu unatakiwa hakuna sababu ya msomi kama wewe kutukana,au kukukashifu imani ya mwenzako. KARIBUN ndugu zangu. "kwa pamoja tujenge nchi yetu,ubaguz mwiko"
 
Ni mahakama inayotumia sheria zilizoko ktk kitabu kitakatifu cha quran katika kutoa hukumu.
 
so why should it be introduced in our country while we are not a non~securalism country??

Kinachokwenda kushughulikiwa au kupatiwa haki na mahakama hii co ufisadi, wizi au jinai nyingine bali kuna masuala yanayowahusu waislamu moja kwa moja kama ndoa na mirathi ambayo hayatakuwa na effect yoyote ktk sheria za nchi. Na kupata haki ktk mahakama hiyo haitalazimishwa eti kwa kuwa ni muislamu bali itakuwa ni hiali ya mtu.
 
Msaada wenu sijui chochote juu ya MAHAKAMA YA KADHI
1.inafanya kazi gani
2.umuhimu wake
3.nini maana yake
 
Kinachokwenda kushughulikiwa au kupatiwa haki na mahakama hii co ufisadi, wizi au jinai nyingine bali kuna masuala yanayowahusu waislamu moja kwa moja kama ndoa na mirathi ambayo hayatakuwa na effect yoyote ktk sheria za nchi. Na kupata haki ktk mahakama hiyo haitalazimishwa eti kwa kuwa ni muislamu bali itakuwa ni hiali ya mtu.

Inapendeza sana umejibu kwa hekma.
 
Back
Top Bottom