Thanda
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 1,915
- 596
Kesi hii ya Kusisimua ilitokea katika mahakama ya kijeshi Nchini na kuibua hisia kali kwa waliokuwa wanaujua ukweli.
Jeshi (Kikosi cha Jeshi-KJ, ambacho ni kikosi cha huduma, na Kikosi cha Vikosi-KV,) vilikuwa sehemu moja na hakuna hata kimoja kilichokuwa na sehemu ya uokaji wa mikate (bakery)hivyo jeshi likalazimika kununua mikate nje, yaani kule SUNKIST.
Quarter Master alikuwa ni afande FULANI, na kwa cheo alikuwa ni Captain. Alichukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo, Afande FULANI aliyekuwa na cheo cha Luteni. Msaidizi wake hakuweza kukaimu nafasi hiyo kwani alikuwa na cheo cha colored seargent/staff seargent.
Karani wa Quarter Master alikuwa ni Lance Corporal (Mwenye V moja) Fulani na ndiye aliyekuwa na jukumu la kusaini delivery note zote.
Ufisadi ulipoanzia:
Jeshi chini ya kamati yake ya bajeti lilikaa na kuona serikali haitakuwa na uwezo wa kila siku kwenda kuchukua mikate, hivyo gari lao itabidi lipunguze safari na kwenda mara tatu kwa wiki na kuchukua mikate ya siku saba. Hapo QM akajitengenezea ulaji. Zile siku ambazo hawaendi akawa anamtuma yule karani aende kule Bakery ya SUNKIST na kuchukua mikate na ama kuiuza kwa wateja wengine au kuipeleka wanakopajua wao. Dili hii alishirikishwa karani wa kule bakery, dada FULANI. Mchezo huo ukafanyika ndani ya miaka mitatu mfululizo na idadi ya mikate ilikuwa ni 700 kila siku. Jeshi likaingizwa kwenye bajeti mara mbili.
Baadhi ya Military Police (MP,s)wakajuzwa kuhusu hilo dili na wakaamua kulifuatiliakwa kumuuliza LC (karani vipi kama dili liko poa na wao wakatiwe kidogo chao. LC akawambia hiyo ishu ni ya bosi wake, QM. Maafisa usalama wa jeshi waakatonywa na kuamua kulishughulikia suala hilo kisomi zaidi kwa kufanya uchunguzi kuanzia kule kiwandani. QM kuona hivyo akaamua kumfungulia mashitaka huyu LC ambaye ndiye aliyekuwa signatory wa delivery note. Jalada likapelekwa kwa Afisa Tawala wa jeshi afande FULANI(Administrative Officer) jeshini huyu huitwa ADMIN. Kwa kuwa naye ni mwanasheria akaamua ku-reason out kuwa haiwezekani ufisadi huu ufanyike kwa muda wa miaka mitatu halafu Quarter Master (QM) asijue. Akaamua kuitisha uchunguzi kwa wote wawili( Lance Corporal Na Captain FULANI). Jalada linapitiwa na Mkuu wa kambi,(Commanding Office-CO) afande FULANI. wote wawili wanasimamishwa kupisha uchunguzi.Lakini kabla ya kuondoka ofisini QM anafanikiwa kuharibu nyaraka muhimi na kuzipoteza, inabaki tu delivery note inayoonesha kuwa mikate iliingia na kutumika. Military Police wakaandaa charge chini ya bosi wao ambaye ndiye mwendesha mashitaka (Prosecutor) na hii ni baada ya ukaguzi wa Wakaguzi wa mahesabu wa jeshi (Military Auditors)kufanyika.
Sheria ya Time Bar inatumika, na kipindi cha time bar kwa jeshi ni miaka mitatu. Hii inaanzia tangu pale mtuhumiwa anapokamatwa na kabla hata ya kupelekwa katika mahakama hiyo ya kijeshi.(Huyu LC alikamatwa tarehe 28 ya mwezi Dec. Jaji wa mahakama hiyo maarufu kwa jina la Marshal Court ndiye rais wa mahakama. Mchezo huu ulikuwa unafamika na Non Commissioned Officers (NCO,s) na hawa ndio waliokuwa watu muhimu kutoa ushirikiano. Baada ya wapelelezi kukosa nyaraka zozote za kuweza kumtia hatiani afande FULANI (QM)wakaamua kupindisha time bar starting date inayosema kuwa inaanzia pale tu mtuhumiwa anapokamatwa wakaibadili na kuifanya iwe inaanzia tarehe 1 mwezi wa kwanza hivyo kuathiri mfumo mzima wa sheria za chombo hicho. Furaha ya QM.....Ikaonekana kuwa mtuhumiwa alibainika kutenda uhalifu kuanzia tarehe 1 ya mwezi wa kwanza, hivyo upelelezi umekamilika tarehe 28 Dec siku aliyokamatwa hivyo kuhukumiwa mapema yaani mwaka wa pili ndani ya time bar.....masikini Lance Corporal (LC) akahukumiwa kifungo cha miezi sita pamoja na kufukuzwa kazi.
Karani wa kule bakery naye hakupona kwani katika delivery note ya jeshi kulikuwa na saini zake. Wakati ambapo huyu LC hayuko basi kitabu hupelekwa na QM ili asaini (fake signature kama ya LC)ingawa sahihi zilikuwa zinafanana kidogo. naye akawa fired (akafukuzwa kazi)
Jumla ya mikate iliyoibwa kwa miaka mitatu:
700breads X 4days a week X 4weeks X 36months =Total 403,200, bei ya mkate ulikuwa ni TSH 370/= hivyo jumla kuu ya pesa za serikali zilizopotea ni takriban THS 149,184,000/=(milioni mia moja arobaini na tisa, laki moja na themanini na nne elfu)
LC amekata rufaa kupitia wakili wa jeshi ambaye naye pia ni Mwanasheria , senior staff, Mheshimiwa Afande FULANI mwenye cheo cha Kanali.(Colonel)akipinga kukamatwa, kushtakiwa, kufungwa na kufukuzwa kazi. Acha tuone kama rufaa itakubaliwa.
Wadau mnaoijua sheria, hii imekaaje?
Usaidizi wa lugha: Richard, Mercy,na Mr Maji