Mahakama yaamuru Marehemu Michael Jackson kumlipa Quincy Jones Sh20.7 bilioni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mtayarishaji nguli wa muziki, Quincy Jones ameshinda kesi ya madai ya Dola za Marekani 9.4 milioni (sawa na takriban Sh20.7 bilioni za Kitanzania) ikiwa ni mrabaha na ada ya kurekodi kazi za aliyekuwa mfalme wa pop duniani, Michael Jackson, magazeti ya Marekani yameripoti.

Jones alifungua kesi hiyo mwaka 2013 akidai Dola za Marekani 30 milioni, lakini Kampuni ya Michael Jackson ikasema kuwa mtayarishaji huyo alikuwa akidai Dola za Marekani 392,000 pekee.

Wiki iliyopita, Jones ambaye anasifika kwa kutayarisha albamu kama “Thriller”, Of The Wall” na “Bad” alisema wakati wa kutoa kiapo kuwa alidanganywa na kuwekwa kando katika mpango wa kutengeneza fedha nyingi, kwa mujibu wa tovuti ya AP.

Baada ya kifo cha Michael Jackson, kampuni iliweka nakshi (remix) nyimbo zake bila ya kumshirikisha Jones ili asistahili malipo ya mrabaha kutokana na nyimbo hizo.

“Mfano mmoja ni filamu ya ‘This Is It,'” alisema Jones. “Jina langu halipo sehemu yoyote karibu na huo wimbo.”

Henry Gradstein, mmoja wa wanasheria wa Jones, alisema Weitzman hakuielewa mikataba ya Jones.

“Mikataba inaeleza kuhusu malipo ya leseni,” alisema. “Kwa miaka 35, pande hizo mbili zimetafsiri kwa njia hiyo na kulipa kwa misingi hiyo. Kusema kwamba ilikuwa zawadi, ni fedheha.”

Tovuti ya Billboard imekariri Jones akisema hukumu hiyo ni ushindi kwa sanaa.

"Kesi hii haikuwa kwa ajili ya Michael, ilikuwa ni kulinda heshima ya kazi tuliyofanya wote katika kurekodi muziki na kumbukumbu ya tulichobuni,” alisema nguli huyo aliyetayarisha wimbo maarufu wa “We Are The World”.

“Ingawa hukumu hii haijatoa kiwango chote tulichodai, nina furaha kwa sababu uamuzi umetunufaisha katika hili. Naungalia ushindi huu si kwa ajili yangu pekee, bali wasanii kwa ujumla.”


mwananchi
 
Anadai hela mifupa ya Michael au? Nielewesheni wabobezi

Wenzetu huko nchi zilizoendelea hakimiliki zinawalinda sana wanamuziki, watayarishaji, watunzi, jingle n.k kiasi ya kwamba hata wakifa wanaendelea kuingia mapesa na wakati mwingine hupata pesa nyingi zaidi wakiwa marehemu kuliko walivyokuwa hai. Mfano USA hakimiliki za wimbo n.k ilikuwa miaka 35 kisha ikaongezwa kufikia 56 na sasa ni miaka 70 ambapo mmiliki wa hakimiliki mfano ametoa kibao chake mwaka 2017 Januari 31 na kufariki kesho yake, hakimiliki itadumu mpaka mwaka 2087 United States Copyright Law - IMSLP/Petrucci Music Library: Free Public Domain Sheet Music .

Kwa Tanzania bado hakimiliki hazipewi heshima ingawa sheria ipo mfano kesi ya MwanaFA & AY kuidai kampuni ya simu za mkononi iliyotumia kibao chao bila makubaliano MAHAKAMA YAAMURU AY & MWANA FA WALIPWE SHILINGI BILIONI 2.1 , sheria ipo sheriayako: IJUE SHERIA YA HAKI MILIKI NA SHIRIKI NCHI TANZANIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…