Harvey Specter
Member
- Jun 26, 2024
- 16
- 16
Mahakama yaiamuru Kampuni ya Safari Automotive Limited kulipa Fidia ya Milioni 10 kwa kusambaza video za mteja wao bila ridhaa yake.
Mahakama Kuu (Masijala ndogo ya Dar es Salaam) yaiamuru Kampuni ya Safari Automotive Limited kumlipa Godwin Danda fidia ya Shilingi Milioni Kumi (10,000,000/=) za kitanzania kwa kusambaza video zake katika mtandao wa Instagram bila ridhaa yake.
Maamuzi hayo yalitolewa tarehe 30 Agusti 2024, na Mh. Jaji David Ngunyale baada ya Rufaa namba 978 ya 2024 iliyofunguliwa na kampuni ya Safari Automotive Limited (Mrufani) kugonga mwamba.
Hapo awali, Ndugu Godwin (Mteja) alifungua kesi ya madai dhidi ya kampuni hiyo katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kupitia kesi Namba 86 ya mwaka 2022 akiidai Kampuni hiyo fidia kwa kuchapisha video yake katika mtandao wa kijamii (Instagram) bila ridhaa yake kwani kitendo hicho kilichukuliwa kuwa ni kuingilia utu na faragha yake bila sababu za msingi kitendo kilichopelekea kuvuruga amani katika familia yake, na kumshushia hadhi, ambapo kampuni iliamriwa kumlipa fidia ya shilingi Milioni Themanini (80,000,000/=) za Kitanzania.
Kampuni hiyo inayojishughulisha na biashara ya kutengeneza vifaa vya magari iliingia makubaliano na mteja huyo ya kuwataka watengeneze viti, dashboard, carpet za 5D na kusafisha gari lake. Baada ya kukamilisha huduma hizo kama ilivyokubaliwa, Mteja alienda kuchukua gari lake ambapo kampuni hiyo ilimrekodi akichukua gari hilo. Video hiyo ilisambazwa mtandaoni kwenye ukurasa wa Instagram wa Kampuni kupelekea Mteja kulalamika kuwa iliathiri utu wake na faragha yake, na hivyo kufungua kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni. Katika shauri hilo, Kampuni ilidai kwamba video hiyo ilirekodiwa kwa ridhaa na haikuwa kwa ajili ya kujipatia faida za kibiashara bali ilitumika kwa lengo la kuelimisha umma.
Mahakama ya Wilaya baada ya kusikiliza pande zote mbili iliamuru Kampuni kulipa fidia ya jumla ya kiasi cha shilingi Milioni themanini (80,000,000) za kitanzania. Hivyo kupelekea kampuni hiyo kukata rufaa katika Mahakama Kuu.
Katika maamuzi ya Rufaa, Mahakama Kuu, iliamua yafuatato:
Kwamba Mteja alikubali kurekodiwa kwa video hiyo, lakini hakuna ushahidi kwamba alitoa ridhaa ya video hiyo kusambazwa Instagram.
Pili, Mahakama ilieleza kwamba kipande hicho cha video kilichosambazwa na Kampuni hakiwezi kutofautishwa na matangazo yake ya biashara kwa sababu maudhui yake yanahusu ubora wa kazi iliyofanywa na Mrufani kwenye gari la Mteja.
Hata hivyo Mahakama ilibainisha kuwa ushuhuda wa wanafamilia wa Mteja huyo haukuonesha madhara yoyote ya dhahiri yaliyosababishwa na kitendo hicho ambayo yangehitaji kiasi kikubwa cha fidia, na hivyo kupunguza fidia hiyo kutoka Milioni 80 hadi Milioni 10 za Kitanzania.
Maamuzi haya yanaenda sambamba na misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kama yanavyoelekezwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kifungu cha 16(1) na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya mwaka 2022 japokua Mahakama haikuongozwa na sheria hiyo katika kufikia maamuzi yake.
Maamuzi haya yakawe onyo kwa wote hasa wauza bidhaa na watoa huduma mbalimbali wenye tabia ya kuchukua picha/video za wateja wao kwa ajili ya kusambaza mitandaoni kama sehemu ya kujitangaza bila kuomba ridhaa kwa wahusika.
Washereheshaji (MCs), Wapiga picha, Wauza nguo na vifaa vya kielekroniki kama simu n.k) Ikumbukwe kutumia taarifa binafsi za watu kama picha na video kwa ajili ya biashara inahitaji makubaliano kutoka kwa muhusika.