JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Jaji David Ngunyale ameahirisha kesi ya Ally Masoud Nyomwa anayejulikana zaidi kwa jina la Masoud Kipanya (KP) dhidi ya Burton Mwemba Mwijaku hadi tarehe 24.9.2024.
Wakili wa Mwijaku (Wakili Patrick Malewo) ameomba kuongezewa muda wa kupeleka Mahakamani utetezi wake wa kimaandishi dhidi ya madai ya KP kwa sababu amesema mteja wake amemuajiari muda wa siku 21 wa kufaili utetezi huo ukiwa umeisha.
Wakili wa Kipanya, Alloyce Komba hakupinga ombi hilo, Mahakama imempa tena Mwijaku siku 21 kupeleka huo utetezi wake.
Kesi itatajwa kwa ajili ya utaratibu wa usikilizaji tarehe 24.9.2024 saa 8.30 mchana.
Wakili Komba amesema Kisheria kesi hiyo inapaswa iishe ndani ya miezi sita (6).
Pia soma:
~ Masoud Kipanya amfungulia Mwijaku Kesi ya Madai ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumtuhumu kufanya biashara haramu
~ Mwijaku aandikiwa hati ya Madai ya Tsh. Milioni 300 kwa kumdhalilisha Maua Sama
~ Mapingamizi ya Mwijaku dhidi ya Masoud Kipanya kusikilizwa Oktoba 17, 2024 Mahakama Kuu