Mahakama yapiga STOP uongozi wa muda NICOL

Mahakama yapiga STOP uongozi wa muda NICOL

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam imeweka zuio la muda kwa uongozi wa muda wa Kampuni ya Uwekezaji ya Taifa (Nicol) kwa kuitaka kutojihusisha na biashara au shughuli yoyote ya kampuni hiyo hadi kesi ya msingi itakapokwisha.

Kesi ya msingi namba 91 ya mwaka 2014, ilifunguliwa na wanahisa waanzilishi dhidi ya uongozi wa muda wa Kampuni ya Nicol.
Uamuzi huo ulitolewa na Jaji wa Mahakama hiyo, John Utamwa, Julai 10, mwaka huu, baada ya kusikiliza maombi yenye namba 297 ya mwaka 2014 yaliyofunguliwa na waombaji; Philemon Mgaya, Thabita Siwale, Ibrahim Kaduma, Balozi Anthony
Nyaki na Sylvester Barongo.

Uongozi wa muda wa Nicol uliopo madarakani, ambao katika maombi hayo ni wajibu maombi, ni Dk. Gideon Kaunda, Elias Mwemezi, Joyce Nyanza, Ladislaus Salema, Elimsaidie Msuri, Emilian Busara na Adam Wamunza.

Wadai hao waliomba yasikilizwe upande mmoja kwa kile walichoeleza kuwa iwapo wangewapa notisi, wadaiwa wangesababisha hasara kwa kutoa fedha nyingi za Nicol benki.

Katika maombi yao, waliiomba mahakama kuwazuia kuhamisha fedha kwa niaba ya Nicol, pia kurudisha Sh. bilioni 1.5 walizolipa katika akaunti, ambayo si ya Nicol, iliyopo Benki ya NMB na kwamba, walisababisha hasara kubwa kwa mali za kampuni hiyo.

Kufuatia uamuzi huo, Jaji Utamwa ameamuru waombaji kuwafahamisha upande wa walalamikiwa uwapo wa shauri hilo.

CHANZO: NIPASHE
 
tobaaaa....................hope NICOL hawatatenda kama ya DECI.................
tumewaamin tumewekeza huko japo ni vya madafu lakin kwa mtu wa kawaida vinamaana sana.
kila nikiskia hii kesi roho inahamalika
 
Nicol ni zaidi ya Deci. Pekua humu Jf kuna topic tumejadili mustakali wa hio 'NGO' tangu kuanzishwa kwake.
 
Nicol ni zaidi ya Deci. Pekua humu Jf kuna topic tumejadili mustakali wa hio 'NGO' tangu kuanzishwa kwake.
sasa wee ndo unataka nikalazwe kwa pb na mtibwa sugar ...........
sitak manake najua nitakufaaaa nihurumie
 
sasa wee ndo unataka nikalazwe kwa pb na mtibwa sugar ...........
sitak manake najua nitakufaaaa nihurumie

Pole mpendwa. Mosha na wenzake wameihujumu sana Nicol. Iko hoi. Please pekua hizo posts usome tuliyojadili. Usikate tamaa mapema
 
Back
Top Bottom