Mahakama yatoa hati ya Wema Sepetu kukamatwa

Mahakama yatoa hati ya Wema Sepetu kukamatwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu yuko matatani baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa hati ya kumkamata kwa kuruka dhamana.

Wema anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani.

Hati hiyo ya kumkamata Wema imetolewa leo Juni 11 mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonda, baada ya upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili Silvia Mitanto kudai kwamba mshtakiwa hayuko mahakamani na hakuna taarifa yoyote.

Wakili wa utetezi, Ruben Simwanza, amedai mshtakiwa alifika Mahakamani lakini kaumwa hivyo ameshindwa kuingia katika chumba cha Mahakama.

Akitoa uamuzi Hakimu Maira amesema Mahakama inatoa hati ya kumkamata mshtakiwa kwa sababu kama alifika alishindwa nini kuingia mahakamani.

Wema anakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono katika mtandao wa kijamii.


Wema anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, ambapo alisambaza video za ngono kupitia akaunti yake ya Instagram, picha ambazo inadaiwa kuwa haina maudhui.
 
Mpaka muda huu ameshaforge makaratasi ya kuumwa.
 
Mahakama zinachosha. Nenda rudi nyingi. Kama uchunguzi haujakamilika kwa nini mnasumbua watuhumiwa? Huku ni kutoa adhabu kabla ya hukumu.
 
sasa hayo maeneo mbalimbali ya dar es salam alikuwa anavua nguo au.... mbona sijaelewa hapo?
 
Inasikitisha sana...

Wakili wake ndiyo kampoteza... alidhani mahakamani ni kama kupita kwenye red carpet...

Wakimaliza na huyo waende kwa Amber Ruti...


Cc: mahondaw
Nadhani kama Unampenda Mwambie Afanye Appearance Mahakamani Tu Hayo Mengine Hayana Maana, Sababu Ya Wakili Kusema Alifika Mahakamani Akaumwa Tumbo Ghafla Na Kuondoka Bila Kutoa Taarifa Mahakamani Sio Hoja Yenye Mashiko, Kuna Mawakili Wanawafanya Wateja Wao Waonekane Vituko @the_originaleast
 
Back
Top Bottom