Mahakama yatupilia mbali pingamizi dhidi ya Lema

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,925
[h=1]MAHAKAMA YATUPILIA MBALI PINGAMIZI DHIDI YA RUFAA YA ALIYEKUA MBUNGE WA ARUSHA MJINI(CHADEMA)GODBLESS LEMA [/h]


Godbless Lema akiwasili katika viwanja vya Mahakama ya Kuu jijini Dar leo.
Wapenzi wa Chadema wakimlaki Mhe. Lema mara baada ya kuwasili katika viwanja vya mahakama leo.
Jopo la Majaji likiwa tayari kuanza kazi.
Kutoka kushoto, Henry Kileo, Nuru Ndosi na Mhe. Godbless Lema wakiwa mahakamani leo.
Henry Kileo akiwa ndani ya ukumbi wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam.
Katibu wa Chadema Kanda ya Kinondoni, Henry Kileo (kushoto) akibadilishana mawazo na mdau wa Chadema mara baada ya kuwasili viwanja vya Mahakama Kuu leo. Habari / Picha kwa hisani ya ARUSHA255
--
Pingamizi lililowekwa na upande wa wajibu rufani kupitia Wakili wao Alute Mughwai ili rufaa ya Lema kupinga kuvuliwa ubunge isisikilizwe limetupiliwa mbali na Mahakama baada ya kuridhika kwamba kosoro zilizolalamikiwa zilikuwa kwa upande wa Mahakama.
Pia kifungu kilichomhukumu Lema kina makosa hivyo kesi itatajwa tena baada ya siku 14 kwa ajili ya kuendelea kusikiliza hoja za waliokata rufaa. Mawakili wa Mhe. Godbless Lema wanahitajika kutimiza mahitaji fulani ya kisheria ndani ya siku 14 ili shauri la rufaa hiyo iweze kupangiwa siku ya kusikilizwa na kuamuliwa.

Wadaiwa kwenye shauri hilo ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi. Lema anawakilishwa na Wakili Method Kimomogoro, anayesaidiana na Lissu.






[h=2][/h]
 
wanachadema mbona mpo wachache au mlienda temeke; labda kesi ihamie Arusha DAR CHADEMA Wababaishaji
 



KUNA TUMAINI LA KUSHINDA KESI HII KWA LEMA LAKINI??
😛eace: 😛eace: 😛eace:
 
tuna imani kubwa sana mh.jaji othumani chande na jopo lake watatenda haki kwa kuzingatia misingi na kanuni za kazi zao bila kusukumwa na itikadi za kisiasa kama tulivyo shuhudia huku mwanzo wa kesi hiyo .
 
Asante kwa taarifa mkuu,bd 2na imani na hii kesi,mungu bariki tanzania mungu mbariki lema.
 
wanachadema mbona mpo wachache au mlienda temeke; labda kesi ihamie Arusha DAR CHADEMA Wababaishaji

Pamoja na kuwa Mh. Othman yuko busy kuwa hataweza kuendesha kesi Arusha but pia ni strategy ya kuipeleka kwa low profile maana kule Arusha ni hatari. Lema atashinda hii Rufaa, subiri utaona.
 
Yule Jaji kihiyo ni miongoni mwa wanaolalamikiwa na Lisu.
 
ashinde ili kuimarisha safu ya mashambulizi (front line)
 
Mahakama ndicho chombo kilichobaki na aibu nchini, lakini vyombo vyote vilivyobaki ni hovyo, hongera majaji kwa maamuzi yenye kuijengea imani jamii dhidi ya mahakama, hongera mahakama hongera Lema.
 
Embu mahakama iturudishe mbunge wetu!Watu wa Arusha tunahitaji kuwa na sauti bungeni!Achen kutupiga danadana wakati kitu kinaeleweka!Hatutaki ubabaishaji wa mambo yasiyokuwa na mantiki!Tunajua ni mwiba wenye uchungu zaidi ya mbigiri kwa mafisadi!Ndiyo ni mwiba!All the best to Lema.
 
Mie si mtaalamu wa sheria lakini kuna mambo ambayo hayahitaji usomee sheria kwa kuwa yako wazi kabisa sasa kwa mfano yale mapingamizi ya Mungwai na wenzake hayajakaa kiuzuri vile yaani kila kitu kipo wazi lakini kwa kuwa wao ni wataalam zaidi so they have to show a bit lakini pale Mh Godbless Lema anarudi Bungeni,Mtaniambia humu humu japokuwa Wabongo ni watu rahisi sana wa kusahau kwa kuwa huwaga tunasoma mambo juujuu na hili ni tatizo sana ndio maana huwaga tunapata viongozi DHAIFU kwa kusahau historia zao kwa kutosoma kwetu na kuweka kumbukumbu.
 

Makamanda mbona mpo wachache hivyo.
 
wanachadema mbona mpo wachache au mlienda temeke; labda kesi ihamie Arusha DAR CHADEMA Wababaishaji

Tuliambiwa humu jamvini kuwa Lema kutikisa Jiji la Dar.
 
Tuliambiwa humu jamvini kuwa Lema kutikisa Jiji la Dar.

Ni kweli katikisa ilikuwa mshike mshike pale mjini! Jamaa anafunika kweli. Si ajabu baadaye akawa rais tuone watafikishana wapi na Heavy Stone (Zitto Kabwe).
 
wachaga sio wengi dar labda kesi ingepelekwa kimara ndo ungewaona wengi hiki chama ni moshi na arusha
wanachadema mbona mpo wachache au mlienda temeke; labda kesi ihamie Arusha DAR CHADEMA Wababaishaji
 
Naamini sheria na haki haviendani,hivyo namwachia Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…