balibabambonahi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 15,771
- 14,294
Kangaroo wote tunamjua,kama siyo kwa kumuona mubashara basi hata kwa picha.Wengi wetu tulianza kumuona kipindi kile tuko kule kwa bibi kijijini Shitimbi,ni mnyama ambaye mara nyingi hubeba watoto wake chini ya tumbo lake ambako ana mfuko fulani.Mara nyingi hunyanyua miguu ya mbele wakati akiruka.
Neno hili limetumika kumaanisha mahakama zenye mrengo wa kupendelea upande mmoja hasa wa watawala.Nitatumia jina hili kuonesha udhaifu katika mifumo yetu ya utawala kama ifuatavyo na kwangu mimi katika muktadha huu nitatumia mahakama za kangaroo kutanabaisha udhaifu katika mifumo yetu ambao umefanya mihimili ya dola kuburuzwa na muhimili mmoja tu wa utawla.
Hivi hizi mahakama haziko Tanzania? Mtu anapotea,inapita miezi kadhaa hajulikani alipo ,taarifa zimeripotiwa polis lakini cha ajabu hadi waziri mwenye dhamana anakiri hadharani kwamba serikali haijui alipo.Haya,maiti zinaokotwa kwenye viroba kila siku lakini kazi ya polisi ni kuzibebe na kuzipeleka kusikojulikana.Kiongozi wa nchi anamuagiza hadharani jaji mkuu aharakishe kumaliza kesi ili serikali ipate pesa ina maana anazi pre empt mahakama,je hii siyo mahakama ya kangarooo? Hapohapo,nafasi ya jaji mkuu inakaimiwa miezi tisa na huyo kaimu anathibitishwa kuwa ndo jaji mkuu,je,hiyo siyo dalili ya mahakama ya kangarooo? Spika ,wakorofi wafukuze bungeni,mimi nitawashughulika huku nje,hii ni kinyume na ibara ya 100 ya katiba yetu.
Bunge linaitikia tu hewala baba,je,hii siyo dalili ya kangaroo? Haya,mbunge anatoka bungeni anakimbizwa na watu wasiojulikana ,mara ,pah! anamiminiwa risasi utadhani digidigi,risasi 38,serikali inaishia kusema ni watu wasiojulikana,ikumbukwe kuwa mbunge huyo alishautangazia umma kwamba anfuatwa na gari fulani ambalo anahisi kuna watu wenye nia ovu dhidi yake.Serikali imepalarize,haichukui hatua hadi mbunge huyu nusura wampore uhai wake.
Kule Mwanza, madiwani walioandamana kudai malipo kutoka mgodini wakakamatwa kwa kula njama, wanamwamrisha kamanda wa polisi akiombe radhi chama tawala,jama! Huu siyo ukangaroo? Kamanda Mawazo na wengine walichinjwa na hakuna aliyekamatwa,hivi kwani mahakama haiwezi kuiamuru serikali kutimiza wajibu wake,na je ile tume ya haki za binadamu ibara ya 129 ya katiba yetu na kazi kama zilivyo kwenye ibara ya 130,iko pale kwa ajili gani?
Mbona haichunguzi na kushtaki matukio haya yanayokiuka haki za binadamu? Vyeti feki vimewaondoa wengi kazini lakini mtu mmoja aliyetajwa kwamba hana vyeti,ameshindwa hata kuonesha vyeti vyake na kila idara ya serikali iko kimya, ama, zimelishwa limbwata aina ya shuntama?