Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Mahakama za mwanzo kuboreshwa
na Mwandishi wetu
JAJI Mkuu mpya, Mohamed Othaman, amesema kazi kubwa iliyoko mbele yake ni kuhakikisha mahakama zinatoa haki kwa wananchi kwa wakati. Jaji Othman alisema hayo jana jijini Dar es Salaam muda mfupo baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Ikulu, Dar es Salaam.
Alisema hata hivyo katika sekta hiyo kuna changamoto nyingi ambazo ni za muda mrefu na kutoa mfano kuwa mahakama za mwanzo ambazo zinahudumia wananchi wengi zinapaswa kuboreshwa ili ziwe na mawakili wa kutosha na wenye ujuzi.
Kwa upande wake, Jaji Mkuu Mstaafu, Augustine Ramadhani, alisema katika uongozi wake amejitahidi kuvunja wigo uliokuwapo kati ya mihimili mitatu nchini ambayo ni serikali, Bunge na mahahama.
Nimejitahidi kuwepo kwa mafanikio kati ya mihimili hiyo, kwani kila siku ya sheria Rais na Spika wa Bunge wamekuwa wakihudhuria tofauti na enzi za Jaji Nyalali, alisema.
Alieleza mafanikio mengine kuwa ni kuanzishwa kwa mfumo wa teknohama, kupatikana kwa majaji wengi na mahakimu kuongezwa maslahi pamoja na paadhi ya kanuni kufanyiwa marekebisho.