Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Aliwahi kuwa rais wa Iran 2005 mpaka 2013. Baada ya kuchaguliwa kuwa rais hakutaka kuhama kutoka katika nyumba aliyoishi. Ilibidi ashauriwe kuhamia Ikulu kwasababu za kiusalama. Alipofika ikulu alikuta zulia la kifahari la Persia lililotengenezwa kwa mkono, aliomba litolewe lipelekwe katika makumbushio ya taifa. Aliomba anunuliwe zulia la kawaida tu kwa matumizi yake akiwa Ikulu
Mahamoud alizaliwa 28, October 1956 karibu na mji wa Garmar huko Iran. Mama yake anatoka kwenye ukoo wa Mtume Mohamad. Walihamia mjini Tehran wakiwa wadogo, Baba yao alipata ajira dukani na aliweza kununua nyumba iliyotosha familia. Watoto walipokua wakubwa baba aliuza nyumba ile na kununu nyumba ndogo. Tofauti ya pesa aliwasaidia wasiojiweza kiuchumi.
Mwaka 1976 alifanya mtihani wa taifa wa kujiunga na elimu ya juu, katika watu 400,000 waliofanya mtihani, alishika nafasi ya 132. Alipata nafasi ya kusoma Civil Engineering undergraduate na hatimae kupata doctorate 1997. Kabla ya kuwa rais alikuwa Prosessor.
Mahamoud anachukia siasa, utamaduni na mawszo ya nchi za magharibi zenye kuendesha siasa za kibepari. Wakati wa utawala wake aliziamuru benki za Irani kupunguza riba wanazotoza kwa 50%. Pia hakuona umuhimu wa matumizi mabaya ya mafuta hivyo kila mwananchi alipewa kiwango cha mafuta anachopaswa kutumia.
Maamuzi haya yalileta mtikisiko katika uchumi wa Iran. Mahamoud hakuwa kikombe cha chai kilichopendwa na wote.
Iran, Kazkanistan na Canada ndiyo wazalishaji wakubwa wa madini ya uranium, madini haya hutumika kama nishati kwenye viwanda vinavyozalisha nguvu na vifaa vya nyuklia. Niger, Urusi, Namibia, China, na Marekani wanazalisha chini ya tani 1,000 za uranium kwa mwaka.