Maharage Chande, mgao huu wa umeme wa mwezi wa saba haukubaliki

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
Kwanza nianze Kusema kuna Mgao wa umeme. Narudia tena kuna Mgao wa umeme.

Napenda kuhoji kwanini Chande Maharage hajatangaza huu mgao wa umeme, ni mara chache mno tunakuwa na mgao wa umeme mwezi wa saba, tunategemea kuwa na mgao kuanzia mwezi wa 10 maana ndo kiangazi kikali kinaanza.

Huyu Maharage mzee wa mifumo ya TEHAMA amefeli kabisa, najua hatuwezi kumlaumu lakini basi japo atupe taarifa kuhusu huu mgao Ili tujipange.

Nasema Kuna Mgao wa umeme, kama unabisha muulize mpenzi wako wa TANESCO.
 
Nakubaliana na mtoa mada kuwa kuna mgao wa umeme.
Niko Moshi - Kilimanjaro.
Juzi umeme ulikatika kuanzia saa 12 jioni hadi saa 5 usiku.
Jana ulikatika asubuhi, ukarudi kidogo mchana, ukakatika tena saa 12 jioni hadi leo haujarudi!
Wakubali tu kuwa kuna mgao, na watoe ratiba ili watu waweze kujipanga.
 
Swala la "TANESCO" lipo Halmashauri Kuu Ya Taifa CCM tunalijadili, tunawaza kuwapa wawekezaji tokea "INDIA" au "CHINA".

Jeshi la Polisi tumeona kuna fursa ya kuweza kutafuta wawekezaji tokea "VIETNAM" au "AFGHANISTAN".

Wananchi msiwe na papara kwa hilo, la bandari tumeshawapeleka Dubai tayari!
 
Jana niligundua hili. Pambav zao
 
Kuna mgao unaendelea, wiki hii niko Arusha umeme unakatika mara kwa mara
 
Kwa hiyo kina cha maji kishapungua mara hii, stiglaz nayo haikujaa! nchi ngumu hii..
 
Swala la "TANESCO" lipo Halmashauri Kuu Ya Taifa CCM tunalijadili, tunawaza kuwapa wawekezaji tokea "INDIA" au "CHINA".

Jeshi la Polisi tumeona kuna fursa ya kuweza kutafuta wawekezaji tokea "VIETNAM" au "AFGHANISTAN".

Wananchi msiwe na papara kwa hilo, la bandari tumeshawapeleka Dubai tayari!
Bunge tafuteni mwekezaji from USA
 
Kwanza nianze Kusema kuna Mgao wa umeme. Narudia tena kuna Mgao wa umeme.

Napenda kuhoji kwanini Chande Maharage hajatangaza huu mgao wa umeme, ni mara chache mno tunakuwa na mgao wa umeme mwezi wa saba, tunategemea kuwa na mgao kuanzia mwezi wa 10 maana ndo kiangazi kikali kinaanza.

Huyu Maharage mzee wa mifumo ya TEHAMA amefeli kabisa, najua hatuwezi kumlaumu lakini basi japo atupe taarifa kuhusu huu mgao Ili tujipange.

Nasema Kuna Mgao wa umeme, kama unabisha muulize mpenzi wako wa TANESCO.
Huwez sikilizwa maan hawajawah kujali kuhusu watanzania, utaimbiwa wimbo wa matengenezo au maji yamekaukaaa 🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom