Gorgeousmimi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2010
- 9,296
- 7,683
Mentor hayo maharage ya mbeya uliyala siku ngapi!!!!!!!!
mbona yamekufanya uwakinai Kibua wako kwa haraka sana!!!!!!!!!
Kumbeeeeeeeeeeeeeeee.......................huna maaaaaaaana hiyo...................basi nimeingi mkengeeeeeeeeeeeeeee!!!!!
nakumbuka mitaa ya maendeleo mbele kidogo ya airport! NIMEPAMISSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS!!!!!!!!!
Mwishoni umeonyesha maana hiyo hiyo.
kweli umeyakomoa ya mbeya..
Yale yanayoliwa kwa staili yake spesho lol...
Hahah...tena sio kuwa KIBUA wakiona kichungu, bali yake miba imekuwa ni kadhia
Heaven on earth puliziiii msaidie dadayo, naona hii siredi iko changanya kabisa medulla oblongata yake...teh teh!!!
HARAGE HALIKOMOLEWIHapa juzi kati nilisafiri kwenda jiji la Mbeya. Kwa kawaida unaposafiri kwenda mkoa tofauti na unapoishi unatamani kula chakula cha watu wa maeneo yale. Mara nyingi huwa ni kutokana na kutaka zaidi kufahamu ladha ya vyakula walivyonavyo wenzetu. Ila pia kukinai na kuchoka kile ambacho umezoea kula huko utokapo.
15th September 2013, Jumapili
Niliwasili mkoani Mbeya kutokea Dar. Barabara safi kabisa hivyo nilifika mapema na wala sikuwa na uchovu kivile. Mara moja nikajitosa mtaani maeneo ya Mwanjelwa..eniwei ndo mjini ukiachia uhindini. Sijawahi elewa hiyo hadhi ya jiji waliipataje but that is a topic for another day, and most definitely not over here, chit chat!
Basi nikawasiliana na baadhi ya wadau wa huku kuona kama tutaonana na kuwauliza ni chakula gani kinapatikana Mbeya ninachoweza kutumia. Member wengine humu ( Heaven on earth, Meritta, Asprin, mwallu, mimi49, Kaizer, Filipo, Arushaone, TheDealer, Mashaxizo, Elli, The Boss et al) pia walinichangia mawazo na katika kufanya mahesabu ya haraka haraka nikagundua wengi wao waliongelea maharage ya Mbeya.
Tena waliyasifia; maharage ya Mbeya bei chee; Maharage ya Mbeya yanaiva haraka; Maharage ya Mbeya hayasumbui kubargain bei; Maharage ya Mbeya mazuri hata kwa sura; Maharage ya Mbeya yanahifadhi joto n.k n.k n.k.
Nami kwa hamu na tashtiti kubwa nikarudi hotelini fasta nikajisafi mwili huyo, Mwanjelwa, maana niliambiwa huko yanapatikana kwa wingi. Nikajiambia by the time naondoka Mbeya lazima nitakuwa nimepata protini ya kutosha na hamu ya maharage itakwisha kabisa ukizingatia sie tuishio Dar ni nadra sana kupata maharage.
Nishazoea kibua changu kwa wali au ugali. Chembamba kirefu ukiwa nyumbani unakiona cha thamani ila subiri hadi uyaone maharagwe ya Mbeya. Kuanzia jioni ile dozi ilikuwa moja. Jioni ni Ugali na Maharage ya Mbeya, Asubuhi ni chai na maharage ya Mbeya, mchana Wali na maharage ya Mbeya. Alimradi kila msosi ulisindikizwa na maharage ya Mbeya.
Nilidhani kwa kula vile ningeyakomoa au walau ningekatisha hamu yote ya maharage niliyokuwa nayo. Nilinunua yote, membamba, manene, meusi, meupe, yale ya soya alimradi ni harage la Mbeya. Samaki na dagaa nilivipita mbali. Maharage ya Mbeya bana
Kuuuumbe kukomoa maharage ya Mbeya ni sawa na kujaribu kukausha bahari kwa sponji. Maharage ya Mbeya hayakomoleki.
Sasa nimerudi kwenye kibua changu nashindwa kula mpaka napatwa wasiwasi yale maharagwe yaliwekewa nini. Kibua kinaniangalia, kimeungwa na nazi na vikolombwezo vyote. Lakini hamu ya kibua imepotea. Tumbo limejaa. Misuli inauma tena imekaza. Nakiangalia kibua changu kwa huzuni nacho kwa jicho moja kinaniangalia. Mpishi naye haelewi Mentor nimekuwaje. Kibua nilichokuwa nakipenda imekuwaje leo hii ghafla hamu imekatika? Mate hayatoki, mdomo haufunguki, ulimi haukazi.
Hamu sina kibua kimeshtukia!
Jamani wakuu chungeni sana maharage ya Mbeya. (ama kwa hakika ni matamu) ila maharage yale hayakomoleki. Kamwe Usidhani utayakomoa Na si maharage tu; Rukwa kuna vibua pia (tofauti na hivi vyetu vya Dar) havina ladha ila ukijiloga ukala bila kumvisha mfuko protini zikaingia tumboni utashangaa unavimbiwa wewe badala yake.
Ntwara kuna korosho. Zina bei kiasi siku hizi nahisi kwa sababu ya biashara ya gesi na watu wengi kuzihitaji haswa Wachina.
Usiende Kigoma ukataka kuikomoa migebuka yao kisa myembamba mirefu meusi na ina sura za kuvutia chunga usijeumia wewe utakaporudi kwenu kwenye mchicha na tembele.
Usile ndizi Bukoba za Wahaya kwa pupa kisa zina maji na ni rahisi kupata na kupika. Tena zaridhisha sana..ila hazikomoleki. .maharagwe kamwe huwezi kuyakomoa.
Ridhika na kibua cha nyumbani kwako isitoshe harage ni harage tu, la Mbeya au la Kahama.
Wakati huu nipo ofisini nikitafakari jinsi ya kuokoa ndoa yangu, mpishi kanuna iweje sina hamu ya kibua!????? Nahisi maharage ya Mbeya yalintia dawa..sidhani kama ni hamira tu!
Wasalaam wapendwa,
Mentor.
NB: Sina maana hiyoooooooo.....
bora umeelewa kichunda...