Bit of some slight business issues here and there but all is well happy to see you around
Hakuna bei gani is right wal bei gani is wrong.(hata angetumia "kiasi gani kinafaa," dhana ni ile ile)
Mahari ni zawadi kimsingi kwa hiyo inaweza kuwa kumfundisha kusoma na kuandika, pete ya bati au shehena nzima abebeshwayo ngamia. Zawadi haiwezi kupangiwa kiasi
Mwanamme anampa zawadi mwanamke kwa kukubali kuwa wake wa milele, kumzalia watoto na hata kuchukua jina lake wakati mwingi mwengine
Hakuna suala la utumwa hapo, mbona mwanamke anabadili jina na kuwa la mwanamme na hawi mtumwa wake?
Hahahahaha... Gaijin umeanza kunichokoza...chokochoko mchokoe pweza...nimekaa Zanzibar wiki mbili utanikoma na maneno yangu sasa hivi :lol::lol:Nimefurahi kukuona, tangu siku nikuwekee "chapati" ukapotea moja kwa moja, au ndo ulienda nawe kugombania? :lol:
Ukubari usikubari hukutakiwa kumuuliza yeye hilo swali,unashangaza!!!
Kama zawadi basi angemwambia "nichagulie unayotaka".
Hili lishakuwa dili sasa.
Na kama zawadi mbona anapewa mwanamke tu?
Hahahahaha... Gaijin umeanza kunichokoza...chokochoko mchokoe pweza...nimekaa Zanzibar wiki mbili utanikoma na maneno yangu sasa hivi :lol::lol:
Ndio hasa msingi uliopo kuwa "nichagulie unayotaka" na mwanamme kwa kujitutumua husema "nitakupa utakacho wewe" ndio akaambiwa bibie anachokitaka.
Kwa hiyo ni suala la kukubaliana baina ya hao wapeana zawadi, kisha kwa wazazi ni kwenda rasimisha na kuthibitishiana mapenzi mbele ya wazazi ......
..........Na mwanamme anapewa, sema kwa siri siri.......:lol:
Hatutaki siri zama za ukweli na uwazi huu.
Ndio maana wengine kuoa tunakusikia kwenye bomba tu, mambo yenyewe biashara ya utumwa?
Vijana inabidi wapelekwe jando kufundishwa uanamume.
Kama wewe hutaki siri, utamwambia akitangaze hicho alichokupa ili wende sambamba na zama za uwazi na ukweli.
Mahari yakifutwa ili kuondoa dhana ya utumwa, na kubadilisha jina kuchukua la ukoo wa mume nako kufutwe ili utumwa umalizike kabisa
Kwa hiyo mwanamme mwenye uanaume hasa haulizi, akiambiwa milioni nne na yeye ana elfu 20 anafanya nini?
Hapa nadhani suala ni unalipa kwa nani? Kama baba wa mtoto na mume mnabadilishana mtoto kwa mahari, inaweza kuwa na mantiki hiyo uliyotaja. Lakini ikiwa ni binti mwenyewe ndie anaepanga mahari, na ndie anaekabidhiwa hicho alichopewa kama tunzo au tunu kutoka kwa mume wake mtarajiwa, sioni ila hapo.
Tukumbuke kuwa mahari si lazima yawe mali.
Mahari kimsingi inategemea watu na watu. Hata wasiokuwa yatima, wenye wazazi wote hai hadi babu na bibi, wapo wanaompa mahari yote anaeolewa.
Kimsingi kwao mahari ni ya anaeolewa (na yeye ndie husema iwe kiasi gani wakati mwengine) na akiamua kuwagaia wazazi wake ni kwa mapenzi yake tu.
Wewe usie jamaa bila ya shaka ni yako wewe na wewe ndie utakaepanga atoe ngapi.
Tangia hapo mi sitaki kumpa jina langu mtu mwingine kama bwana wa mtumwa.
Mwanamme mwenye uanamme hasa atajua anasimama wapi.
Ama mambo ya upuuzi wa mahari hayataki na atachagua mwanamke wanayeendana naye asiyetaka kulipiwa mahari.
Ama kama anayataka atajua kwamba huyo mwanamke wake "chuna buzi" si mtu sahihi wa kumuuliza hilo.
Watoto hawa wanavamia mambo kwa pupa.Usikute hata neno "mshenga" halijui.
Mie abadan habari hizi.
Nyinyi ndo mnaiharibu dhana nzima ya mahari, mie nataka kudai kutungiwa shairi, hapo chuna buzi imehusikaje?
Nijuavyo mimi mahari hutolewa kwa familia ya binti na mara nyingi baba hupokea kwa sababu yeye ndiye huhesabika kama kiongozi wa familia.
Sijawahi sikia binti akipanga na kupokea mahari mwenyewe. Ni utaratibu wa wapi huo?
Una mfano wa jamii ambazo kwao hawatoi mahari ambazo ni mali?
Hivi anayeolewa zaidi ya mara moja naye anatakiwa kupokea mahari kwenye kila ndoa mpya?