Mahari kubwa yamkosesha mke

Pengine ni wewe
Muhimu utambue kuwa kama unamuhitaji huyo ongea nae vizuri awaeleze hao wazee kuwa yeye hauzwi. Wakikataa mil 2.5 anaondoka kwao. Ila akiendelea kusema yuko na nduguze, basi kubali tu huyo si wako. Hata ukidhalipa mil 5 mfano, andaa tena mil 5 kufanikisha ndoa
 
Mahari kama kununua kirikuu!
 
Hakuna mwolewaji hapo. Atulize akili apate mwingine mbona wanawake wapo wengi tu wanaojielewa.
 
Kwenye familia zenye ustaarabu kupungukiwa mahari hakuwezi kumkosesha kijana mke hata siku moja. Hiyo familia itakua ni zile familia za ajabu ajabu tu. Huyo kijana hata kama angekua na hiyo pesa, ingekua ni kilio kikuu kwake kuoa mwanamke kutoka familia ya ajabu kiasi hicho.
 
Hilo jambo lishanitokea tena hivyo hivyo nilimtema huyo dada mpka leo nilioa mwingine.
 
Mahari ya 5m kwa kipi hasa? Ndoa zenyewe tia maji hizi, mwanamke umekutana nae ukubwani wakubwa walishatanua njia, hakuna bikra na kidume utoe 5m, ni ujinga uliopitiliza.

Kwanza hiyo 500k waambie wairudishe ili kama mchakato hauendelei usipate hasara. Mahari isizidi 2m maana there's nothing new utakiona kwa bidada.
 
Mahari kibongobongo hazifuati dini za wahusika bali mila za kabila na ukoo huo.
Mwache aropoke! Na nyie vijana kama unaona hiyo mila huiwezi si mkaoe kwenye makabila yenu ambako mila zinaendana? Ila hiyo familia nayo itakuwa inaendeshwa na mama, Siku hizi mbona mahari inapangwa na binti mwenyewe? Usukumani hakuna mila ya kishika uchumba ya laki 3. Hizo laki 5 zilikuwa za nini? Kama walisema ng'ombe 10, kwa pesa Usukumani hiyo ni milioni 2 sasa huyo ng'ombe wa laki 4 ametoka wapi?
 
Kama anajimudu na amependa sana awalipe zote,aoe binti huyo,akishamuoa tu,awafungie vioo na asijiweke karibu na familia ya mwanamke,na asijihushe na jambo lolote lile kuhusu familia ya mwanamke,iwe msiba, shughuli au matatizo mengine, kikubwa mwanamke aheshimu maamuzi yake mwanaume kama sasa hivi anavyoheshimu maamuzi ya familia yake kwenye kupanga hiyo mahari.Ndoa ni undugu,sasa kama hiyo familia haitambui hilo ni kunyooshana tu,ila mwanamke atakapo taka kwenda kwao ampe uhuru wa kwenda muda wote ule akawasalimie ndugu zake na wazazi wake,asimkataze.maana wengine wakifanyiwa hayo matendo wakati wa ulipaji mahari hawataki hata binti akasalimie kwao.
 
chamaana mpige mimba ya mapacha mbona hyo laki tano watarudisha watakuomba ukae na binti yao bure
Hiiiiiiiiii! Hiith, Hiith, Hiith nimekuita mara tatu, huo mchezo kuna jamaa yangu alijidai kuufanya ili awakomoe wazee, baada ya mpachiko akaruka weeeee, jongoo liligoma kupanda mtungi mpaka kesho kutwa! Ogopa watoto wa watu huwezi kujua kanajiamini nini hako kazee!
 
Kwanza sasa hivi kwa maisha haya ya uswahilini ukitajiwa mahari above 1.5M ,geuka nenda katafute mchumba kwengine uoe.mahari ipo pale kwa ajili ya kuhalalisha ndoa,na sio biashara
 


Asije oa hiyo sonyela.
 
Wazazi wake wanamponza binti yao.....ila pia huwezi jua wameona nini kwa huyo kijana.....mambo yao tuwaachie wenyewe
Waone nini bhana hao wazazi? Ni wahuni tu, mtoto amesoma mpaka ana kazi yake amepata mchumba amempeleka kwao, unafikri yeye hajaviona vyote kwa huyo kijana? Hawa ndo aina ya wazazi wanaoharibu maisha ya watoto wao kwa kujifanya wajuaji.
 
Sasa hapo si hana pesa,Wasukuma mwenye dau kubwa ndio anaoa binti akilazimisha atakula bakora Hadi akome
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…