Mahesabu yampa ushindi Freeman Mbowe, atarajiwa kuridhiana na Tundu Lissu

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,358
Hayawi Hayawi sasa yamekuwa.Mkutano Mkuu wa Chadema uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu umewadia. Ni hapo kesho kutwa tarehe 21 Januari, siku ya Jumanne.

Hakika yamesemwa mengi na kampeni za kuwania kuingia ofisi Kuu ya Mikocheni zimepamba moto na sasa ni lala salama.

Vyovyote iwavyo Chadema imeweza kutikisa nchi na mamilioni ya watu kila siku wanafuatilia kinachoendelea katika chama hiki kikuu cha upinzani.Kwa asilimia kubwa chama hiki kimeweza kuonyesha kwa vitendo demokrasia wanayohubiri .

Kumekuwa na dosari kadhaa katika kampeni za mafahali wawili Freeman Mbowe na Tundu Lissu na dosari kubwa zimesababishwa na wapambe wa pande zote mbili pale wanaposhindwa kunadi wagombea wao kwa kutumia sera zao bali wanajikita kushambulia na kuchafua wapinzani wao, hiyo ndiyo dosari kubwa ambayo inatakiwa kutizamwa chaguzi zijazo.

Molemo Media chombo huru kabisa kimefanya tathmini karibu majimbo yote nchini kwa kuwatumia watu huru wasioegemea upande wowote kuona mwenendo wa uchaguzi na kwamba wajumbe wa mkutano mkuu watamchagua nani siku ya tarehe 21

TImu ya Molemo Media imefanikiwa kupata idadi kamili ya wapiga kura wa mkutano mkuu kama ifuatavyo;

1. Majimbo ya Uchaguzi 264×3 = 792
2.Wilaya za kichama 64×2 = 124. 3.Mikoa ya Kichama 34×2 = 68
4. Kanda za Kichama 10×3 = 30
5. Mabaraza: BAWACHA, BAZECHA na BAVICHA Jumla wajumbe 99
6. Wajumbe wa Kamati Kuu: 15.

Kwa hiyo, jumla ya Wajumbe wanaotazamiwa kushiriki mkutano mkuu ni 1,328/=

Molemo Media imefanikiwa kujipenyeza na kupata uhakika wa mwelekeo wao kutoka kwa wajumbe wa mkutano mkuu, kwa timu ya kampeni ya Freeman Mbowe na timu ya kampeni ya Tundu Lissu pia kwa viongozi kadhaa wa makao makuu.

Kutokana na tathmini hiyo Molemo Media inaweza kuthibitisha bila wasiwasi wowote kwamba Freeman Mbowe atachaguliwa kwa mara nyingine kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema kwa kipindi cha 2025 - 2029 kwa ushindi usiopungua asilimia 60%

Molemo Media imeweza kugundua udhaifu wa timu ya kampeni ya Tundu Lissu ambapo wamekuwa wakijikita na kuitisha mikutano ya waandishi wa habari mikoani na majimboni na kuwakusanya wanachama wa kawaida wasio wapiga kura na kutoa matamshi makali ya kumuunga mkono Lissu na kutishia kuhama chama endapo Lissu asiposhinda.

Timu ya Freeman Mbowe wao wamekuwa hawazungumzi sana bali wanajikita vijijini kutafuta kura kimya kimya na kuhakikisha namba zinasoma upande wao.

Wanachadema wengi na Viongozi kadhaa waliozungumza na Molemo Media wamefurahishwa na sera ya Freeman Mbowe ya kuanzisha Tume ya ukweli na Upatanishi ambayo itatumika kuponya majeraha yaliyotokana na uchaguzi mkuu wa Januari 21.Katika hali hii Fresman Mbowe anatarajiwa kuitumia Tume hii kuweza kuridhiana na mpinzani wake mkuu Tundu Lissu ili maslahi ya chama yapewe kipaumbele.

Yote kwa yote msema kweli ni Januari 21 ambapo Mkutano Mkuu utakutana kumchagua Mwenyekiti mpya wa Chadema.

Molemo Media inautakia kila la kheri Mkutano Mkuu wa Chadema 2025.
 
Maridhiano CHADEMA!🤣🤣🤣🤣🤣
 
mfahamu sultan ibn mbowe king'ang'anizi
IMG-20241206-WA0083(1).jpg
 
Sema tu hayo ni matamanio yako,ila yote kwa yote tuwaachie wajumbe watufanyie kazi hii kulishana matango pori ni tatizo lingine kwani matokeo yakiwa kinyume na matamanio yenu mtaanza kupiga mayowe busara ni kuwa na subira wajumbe wafanye kazi yao.
 
Hii ni chai mkuu
 
Imebaki siku moja tu, ili tujue mbivu mbichi. Tuwe na subira ndugu Watanzania.
 
Back
Top Bottom