Kenya; Gun Facts Figure and the Law
Uganda; Gun Facts Figure and the Law
Tanzania; Gun Facts Figure and the Law
Ethiopia; Gun Facts Figure and the Law
Mkuu kilam, data sources nilizotumia hizo hapo juu. Ukiwa na data tofauti za kwako pia unaruhusiwa kuweka papa hapa.
“If we have data, let’s look at data. If all we have are opinions, let’s go with mine.” – Jim Barksdale, former Netscape CEO.
Hizi ni annual homicides by GUNS only. Ndio maana pale juu nikasema Kenya might still have much more homicides based on other types of weapons. Hata ngumi zinaua.Ni "annual homicides by any means" au by gunshots?
Hizi ni annual homicides by GUNS only. Ndio maana pale juu nikasema Kenya might still have much more homicides based on other types of weapons. Hata ngumi zinaua.
Soma vizuri hizo link zako.
Okay shukrani dear neighbour. I like to hear these stories unfortunately kuna msee hapa kasema waTz tuko so obsessed na Kenya.Kwanza kabisa kama unataka kuwa wakili kama unavyosema, basi ni muhimu sana ukaanza kwa kurekebisha uandishi wako, matumizi ya herufi kubwa kwenye kila neno sio utaratibu unaoruhusiwa kifasaha.
Tukija kwenye mada husika, hayo mambo ya Hessy hayatendeki Nairobi yote, ni baadhi ya vituko vya uswazi. Binafsi nikiwa kijana hustler mjini kuna kipindi niliishi uswazi Nairobi na kuna askari mmoja alikua na hulka kama za huyu Hessy. Yeye alikua anawapa washukiwa nauli kwamba warudi kwao vijijini, na yeyote aliyekiuka aliishia kuuawa akiwa kwenye harakati za ujambazi.
Huyo polisi alikua kila akikuonya, anaanza michakato ya kukuwinda hadi pale atakukuta ukitenda uhalifu na atakuulia mbali bila kupepesa macho. Nakumbuka kipindi fulani alimuonya jamaa awache ujambazi na akampa nauli arudi kijijini, jamaa akakiuka na kuendelea na uhalifu, sasa askari akamuwinda bila kufanikiwa, japo aliendelea kusikia sifa za jamaa alivyokua anafanya ujambazi. Siku moja wazazi wake jamaa ambao walikua wanaishi mjini pia, wakamtembelea huyo askari na kumwomba asamehe mwana wao. Yeye akajibu kwamba yupo radhi kumsamehe ila waandae kitita cha hela za kumhonga na kwamba wakutane wote na mshukiwa ili waongee jinsi ya kusuluhisha, akawaomba waandae elfu hamsini za Kenya, kama zaidi ya milioni moja za Bongo.
Baada ya hapo wazazi wakakusanya hela na kumpa askari, na wakaita kikao kati yake na mshukiwa, walipokutana, jamaa aliwaskliza wote akiwa kimya, ghafla akanyanyuka na kuchomoa bastola na kumwulia mbali mshukiwa mbele ya wazazi wake. Halafu akarejesha hela zao na kuwaambia wazitumie katika kusafirisha maiti hadi kijijini ili wakamzike bila gharama zaidi.
Huyo askari tulikua tunampenda sana huko gheto, alikua komando wetu maana jamaa alikua na utashi wa kazi yake. Nakumbuka alivyokua anaamka mapema saa kumi za usiku na kujichanganya na wauza maziwa kitaa, akijifanya na yeye ni mchuuzi wa maziwa pia. Kwa mtindo huo alikua akiwaibukia majambazi kiulaini na kuwapa risasi za ghafla.
Mwisho wake ulifika siku alimpiga risasi mtoto wa kiongozi fulani, ambaye mwanaye alijiingiza kwenye uhalifu baada ya kuwa teja. Alihama kwao maeneo ya kifahali kule Karen na kuanza kuishi uswazi huku akiwa teja na kuhusika na uhalifu, baada ya askari komando wetu kumpiga risasi, wazazi wa jamaa wakacheza figisu figisu askari wetu akaishia rumande. Tuliandamana kwa fujo lakini ndio hivyo tena, hapakua na jinsi wala nini, kuna watu wasioguswa dunia hii.
Hivyo nikihitimisha, wapo maaskari kama huyo Hessy wasioangazwa kwenye vyombo vya habari na wanapendwa sana uswazi. Lakini sio kweli mlivyoaminishwa huko Tanzania eti ukija Kenya utakufa mara moja kwa kupigwa risasi.
Then it seems the problem is much deeper. According to the data Kenya is indeed much safer in the EA region.
Okay Nimekuelewa.Maybe uchunguze borders za Kenya na South Sudan, Southern Ethiopia, Western Uganda and Somalia. Kenya imezungukwa na nchi nyingi ambazo zipo vitani au zina maeneo ambaza zina mrundiko wa silaha mikononi mwa raia. The only functional borders ni ya Tanzania na South Western Uganda.
Kwa kawaida maeneo kama haya, kuzuia silaha kuingia nchini ni kazi kweli kweli. Inaonesha state capacity ya Kenya as a nation ni nzuri kwa kuwa Kenya imekuwa na maendeleo muda huu wote ilhali majirani zake ni wa aina hii. Sio nchi nyingi huzingirwa na so much turmoil na zikabaki salama.
Ukifanya research kidogo utakuta kwamba kati ya nchi za Afrika Mashariki Kenya inakadiriwa kuwa na silaha 680,000 ndani ya mipaka yake. Gun deaths (Total homicides au vifo vinavyosababishwa na silaha hizo) ni 2,761. Ukilinganisha na nchi zingine za ukanda huu, Kenya ina silaha nyingi lakini vifo vinavyotokana na silaha hizo ni chache. Mfano Ethiopia ina silaha 320,000 na vifo 11,048 wakati Tanzania ina silaha 550,000 na vifo 6,071, Uganda idadi silaha ni 400,000 na vifo 3,753.
Nadhani sababu kubwa ya kuonekana kuwa Kenya ina gun problem ni aina ya uandishi wa habari. Kenyan news ziko a bit more sensational kwa hio mauaji/ukame etc kuliko her neighbors.
Okay Mkuu. I Understand You. Hizi Gangs Sio Nzuri Kabisa Kwa MaYouth.Guns are not that easily accessible as mobile phones in Kenya. Those kids obtain guns, not by buying them from stores. In fact, they do not even own them.
These kids upon being inducted into the criminal gangs, are provided these weapons by the gang leaders who themselves obtained these guns from some underground criminal organizations importing these weapons from countries such as Somalia and Sudan, where there is such an influx of small arms due to the raging comflicts in those places.
Hahahahahahahaa. Mie Mtz Kabisa. Panya Road Wajinga Hawana Hata Strategies Pumbavu!Nilikuwa na shauku kuhusu uraia wako jombaa lakini nimedhibitisha we mtz nilivoona tu umetumia neno nawaboa,wakenya hawalitumii neno hilo kamwe.Kwa sheng wanasema nawabooh,unabooh,mnabooh si kuboa.Sawa,mimi mwenyewe fan wa crime fiction vitabu lakini,si movie.Crime kule Eastlands ishakuwa ni fiction jombaa ni hatar si siri!Leo ukiona kwa fb Hessy wa Dar utaskia kwenye nyuz panya road mkuu kauwawa!
So Sorry Msee!Yeah, I have realized that. But when was trying to read his initial post, I found myself distracted by the numerous caps within the text. It is as hard to read as when a long text is in all caps. I just couldnt read past the few lines.
So, I had to copy- paste that cluttered epistle into the word document, removed the caps, introduced the paragraphs....and the jamaa actually had interestings things to say contrary to my initial impression.
Kwani Za Tz Nimesema Sifuatilii Kaka?what do you mean Real Life Events? crime iko kila mahali... mbona uConcentrate na issues za Kenya?
Hahahaha. Kwaiyo Mimi Ni Kiongoz Wa Gang Au??Mosi ,Juan Moses siyo mtanzania Juan Moses is an impostor. Pili, criminal gangs to tishio kubwa baadhi ya mitaa hadi kuwakosesha wananchi amani. Bila "summary dismissal" criminals gangs were taking over estates with impunity,maiming killing robbing innocent wananchi. Hanna jinsi zaidi ya kuwafagia. Watajuahawajui tu.
Na Wa Dandora??Hessy wa Kayole is doing a commandable job. Hessy superman wa Nairobi protecting the law abiding citizen.
Sema hayo ndiyo unayoyafaham sio mnayoyafaham, huwezi kuongelea nafsi za watu wengine!Omwami, nakuita hilo jina maana uliniambia umetokea Kagera, hivyo aidha utakua Mhaya au Mnyambo ambao wana undugu na Waluhya wa Kenya akina NairobiWalker wao hutumia hilo Omwami na nilikuta linatumika kwenu.
Anyway, nikija kwenye kauli yako, sidhani kama kuna Mtanzania asiyeijua Kibera, hili neno Kibera limeenea hadi vijijini Tanzania. Hutumiwa sana kuwapa 'feel good mentality' kila mnapohoji kwanini Kenya imeishinda Tanzania kiuchumi, huwa kitu cha kwanza cha kuwaliwaza kwamba Kenya kuna umaskini mwingi na Wakenya mamilioni wanaishi Kibera hivyo mnatulia na kuacha kuhoji zaidi.
Kuhusu ufuatiliaji wa masuala ya Tanzania, kuna idadi ya Wakenya wanaopenda nyimbo zenu, hilo nakiri, haswa Wakenya wa maeneo ya Pwani ambao wana undugu na Watanzania wa Pwani na Tanga. Kingine ambacho Wakenya wanakifahamu sana kutokea Tanzania ni uganga, maana Kenya kuna mabango mengi sana ya waganga wenu. Halafu Wakenya wanawafahamu sana Watanzania kwa kupenda kuomba omba maana ndugu zenu wamejaa kwenye pembezoni mwa barabara zetu wakiomba omba.
Hatimaye Wakenya wanawajua sana Watanzania wenye asili ya Kichagga maana hawa jamaa hujituma sana Kenya na ni wajasiria, wapo wengi kwa maelfu, ukienda sehemu inaitwa Gikomba utadhani upo Moshi maana ndio wengi hapo. Japo kuna wale wamewekeza hata kwenye soko la ujenzi, jirani yangu Mchagga amejenga apartments za nguvu.
Sasa hayo ndio tunayoyafahamu kwa sana kuhusu Tanzania, japo Wakenya wazee wanamjua sana Nyerere lakini sio kwa vijana. Labda Magufuli siku hizi maana amengazwa sana kwenye hilo la kutumbua na kubana matumizi. Zaidi ya hao labda kwa Mkenya kama mimi ambaye nimekatiza vijijini kwenu, nimeingia mitaani, nimesafiri wilaya na mikoa mingi sana huko hivyo nimekua na muda wa kufuatlia hata siasa zenu kwa kina.
Lakini ukiingia upande wa Tanzania, wengi mnafuatlia sana mambo ya Kenya, sijasema ni vibaya lakini ndio hali ilivyo. Binafsi nikiongea Kiswahili ni vigumu kughamua asili yangu kwa lafudhi, hivyo huwa nikijichanganya na Wabongo bila wao kunishtukia, halafu nawakuta kwenye vijiwe wakijadili Kenya hadi napata raha. Kuna maeneo mengi sana nilishawakuta mkijadili Kenya na Wakenya na siasa za Kenya, ila wengi huwa wanasifia na sio kuponda.
Kwanza nilikuta wengine wanabishana balaa kuhusu siasa za Kenya, na huwa sijitambulishi ila nawaskliza tu kimya kimya na kucheka kimoyo moyo.
Halafu kwenye runinga mara nyingi unakuta mpo kwenye Citizen ya Kenya ambayo ni maarufu sana huko.
Sema hayo ndiyo unayoyafaham sio mnayoyafaham, huwezi kuongelea nafsi za watu wengine!
Na kama hujui vingine kuhusu Tanzania (japo naamini unajua na dhamira yako inakushuhudia) hiyo ni kutokana na aina yako ya maisha!
Wewe unatwambia hujui kitu wakati mkenya mwenzio hadi anajua idadi ya vifo vitokanavyo na siraha Tanzania! Upuuzi gani huu
Kama ilivyo kawaida yenu, nyie husoma bandiko na kukimbilia kujibu bila hata kutumia walau dakika moja ili utafakari mwandishi ameandika nini na alikusudia kusema au kumaanisha nini. Naomba urudie nilichokiandika hapo, soma mara kadhaa halafu uje upya maana hamna sehemu nimesema kwamba sina ufahamu wa Tanzania.
Binafsi naifahamu nchi yenu vilivyo, nimekatiza maeneo mengi sana zaidi ya wengi wenu, lakini kabla ya hapo sikua naifahamu zaidi ya Wakenya wa kawaida. Nimeorodhesha vitu vya msingi wanavyovijua Wakenya kuhusu nchi yenu.
Huku Kenya tumezoea kuona mabango kama hili hapa
View attachment 517682
Au taarifa kama hizi
Nahisi wewe ndo hujasoma vizuri makala yangu fupi,Kama ilivyo kawaida yenu, nyie husoma bandiko na kukimbilia kujibu bila hata kutumia walau dakika moja ili utafakari mwandishi ameandika nini na alikusudia kusema au kumaanisha nini. Naomba urudie nilichokiandika hapo, soma mara kadhaa halafu uje upya maana hamna sehemu nimesema kwamba sina ufahamu wa Tanzania.
Binafsi naifahamu nchi yenu vilivyo, nimekatiza maeneo mengi sana zaidi ya wengi wenu, lakini kabla ya hapo sikua naifahamu zaidi ya Wakenya wa kawaida. Nimeorodhesha vitu vya msingi wanavyovijua Wakenya kuhusu nchi yenu.
Huku Kenya tumezoea kuona mabango kama hili hapa
View attachment 517682
Au taarifa kama hizi
mkuu una kiswahili kizuri, nahisi utakuwa umekaa bongo kidogo wewe!Kwanza kabisa kama unataka kuwa wakili kama unavyosema, basi ni muhimu sana ukaanza kwa kurekebisha uandishi wako, matumizi ya herufi kubwa kwenye kila neno sio utaratibu unaoruhusiwa kifasaha.
Tukija kwenye mada husika, hayo mambo ya Hessy hayatendeki Nairobi yote, ni baadhi ya vituko vya uswazi. Binafsi nikiwa kijana hustler mjini kuna kipindi niliishi uswazi Nairobi na kuna askari mmoja alikua na hulka kama za huyu Hessy. Yeye alikua anawapa washukiwa nauli kwamba warudi kwao vijijini, na yeyote aliyekiuka aliishia kuuawa akiwa kwenye harakati za ujambazi.
Huyo polisi alikua kila akikuonya, anaanza michakato ya kukuwinda hadi pale atakukuta ukitenda uhalifu na atakuulia mbali bila kupepesa macho. Nakumbuka kipindi fulani alimuonya jamaa awache ujambazi na akampa nauli arudi kijijini, jamaa akakiuka na kuendelea na uhalifu, sasa askari akamuwinda bila kufanikiwa, japo aliendelea kusikia sifa za jamaa alivyokua anafanya ujambazi. Siku moja wazazi wake jamaa ambao walikua wanaishi mjini pia, wakamtembelea huyo askari na kumwomba asamehe mwana wao. Yeye akajibu kwamba yupo radhi kumsamehe ila waandae kitita cha hela za kumhonga na kwamba wakutane wote na mshukiwa ili waongee jinsi ya kusuluhisha, akawaomba waandae elfu hamsini za Kenya, kama zaidi ya milioni moja za Bongo.
Baada ya hapo wazazi wakakusanya hela na kumpa askari, na wakaita kikao kati yake na mshukiwa, walipokutana, jamaa aliwaskliza wote akiwa kimya, ghafla akanyanyuka na kuchomoa bastola na kumwulia mbali mshukiwa mbele ya wazazi wake. Halafu akarejesha hela zao na kuwaambia wazitumie katika kusafirisha maiti hadi kijijini ili wakamzike bila gharama zaidi.
Huyo askari tulikua tunampenda sana huko gheto, alikua komando wetu maana jamaa alikua na utashi wa kazi yake. Nakumbuka alivyokua anaamka mapema saa kumi za usiku na kujichanganya na wauza maziwa kitaa, akijifanya na yeye ni mchuuzi wa maziwa pia. Kwa mtindo huo alikua akiwaibukia majambazi kiulaini na kuwapa risasi za ghafla.
Mwisho wake ulifika siku alimpiga risasi mtoto wa kiongozi fulani, ambaye mwanaye alijiingiza kwenye uhalifu baada ya kuwa teja. Alihama kwao maeneo ya kifahali kule Karen na kuanza kuishi uswazi huku akiwa teja na kuhusika na uhalifu, baada ya askari komando wetu kumpiga risasi, wazazi wa jamaa wakacheza figisu figisu askari wetu akaishia rumande. Tuliandamana kwa fujo lakini ndio hivyo tena, hapakua na jinsi wala nini, kuna watu wasioguswa dunia hii.
Hivyo nikihitimisha, wapo maaskari kama huyo Hessy wasioangazwa kwenye vyombo vya habari na wanapendwa sana uswazi. Lakini sio kweli mlivyoaminishwa huko Tanzania eti ukija Kenya utakufa mara moja kwa kupigwa risasi.
Hessy is actually agroup and not a personHessy wa Kayole is doing a commandable job. Hessy superman wa Nairobi protecting the law abiding citizen.