Mahindi yangu nitauza wapi

Mahindi yangu nitauza wapi

Maundumula

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
7,553
Reaction score
3,081
Habari zenu wandugu,

Kwanza nashukuru kwa kunipa hamasa ya kuingia kwenye kilimo.

Inshallah mambo yakienda vizuri nategemea kuwa na mahindi kama gunia 800 au zaidi mwezi wa saba mwaka huu hapo Bagamoyo

Naomba kujua nitauza wapi haya mahindi?, kama wateja wapo ikifika wakati naomba tuwasiliane.
 
Hongera sana, mkuu ila unaweza
1. uza kwa wanunuzi

2. unaweza process na kuuza unga na pumba

3. uaweza fikilia kuwa na kiwanda chako kwa baadae cha kuprocess hayo mahindi au hata chakula cha kuku.

Ila kwa gunia 800 maana yake inabdi ununue kwa majirani kuongezea
 
Hongera sana. Mie nakushauri kama kuuza wakati wa kuvuna, uza kidogo sana. Vinginevyo andaa store yakae uuze kuanzia November hadi April mwakani. Vinginevyo nunua au yapeleke mashine za Hill Mapinga saga unga uuze kwenye maduka au sokoni. Ungekuwa mfugaji ndio fursa ya kuyatumia kwa mifugo yako. All the best
 
Mama Joe,

Tatizo sina pa kuyaweka ningependa niyaweke lakini italeta shida nimepiga hesabu chap chap naweza kuingia gharama kubwa nikikodi eneo.
 
Kama ni hivyo anza kutafuta soko kwa kina Bakhressa, wenye mashine za kusaga kama huyo Hill inakupunguzia gharama usafiri.
Ila nafikiri uulizie soko la unga ujaribu kusaga na kuuza bila kuhifadhi, mfano ukipata oda kiasi hiki unaongea mashine unasaga unapack na kupeleka. Jaribu option tofauti lakini ukiprocess ndo faida zaidi.

Wacha nijaribu kufanya hivyo.

Mimi ndio nimeanza kwahiyo mengi haya siyajui hata.
 
Habari zenu wandugu,

Kwanza nashukuru kwa kunipa hamasa ya kuingia kwenye kilimo.

Inshallah mambo yakienda vizuri nategemea kuwa na mahindi kama gunia 800 au zaidi mwezi wa saba mwaka huu hapo Bagamoyo

Naomba kujua nitauza wapi haya mahindi?, kama wateja wapo ikifika wakati naomba tuwasiliane.

Hayo mahindi kidogo sana, peleka pale sokoni Tandale, usipoteze muda hata kwenda Kariakoo!
 
kwanini usianze na kuuza mabichi?...
tena kwa bagamoyo to dar hakuna gharama kubwa za usafiri which means

utapata faida kubwa sana waweza uza mabichi kwa sasa NA KIBARIDI HICHI KUNA FAIDA
 
Ungekuwa Kanda ya Ziwa mahindi yako yangeuzika kwa urahisi sana. Mwaka huu jirani zetu wa Kenya wana njaa kali sana. Kwenye mwezi wa nane au wa tisa gunia moja la mahindi linaweza kuuzwa Tshs.100000 pale mpakani. Nakushauri uendee uongee na Bakressa ili ayanunue kwa ujumla ingawaje wafanyabiashara wakubwa wanaringa sana wapoona umeenda kuwapigia magoti ya kuuza mahindi yako. Huu ndiyo ubaya wa monopoly.
 
kwanini usianze na kuuza mabichi?...
tena kwa bagamoyo to dar hakuna gharama kubwa za usafiri which means

utapata faida kubwa sana waweza uza mabichi kwa sasa NA KIBARIDI HICHI KUNA FAIDA

Nilifikiria wazo la kuyauza mabichi ambayo inafaida kubwa lakini nikasita maana nikianza kuvuna wasije wanakijiji wakasaidia kuvuna zaidi ikaleta shida.
 
mabichi yanafaida sana,vipi canter zinafika shambani? kama zinafika mvua haijaalibu barabara,uza mabichi
 
Nilifikiria wazo la kuyauza mabichi ambayo inafaida kubwa lakini nikasita maana nikianza kuvuna wasije wanakijiji wakasaidia kuvuna zaidi ikaleta shida.

mkuu kwani unavuna limoja limoja si unavuna mengi kwa pamoja
 
Mmmm hili nalo neno, kwavile unaanza sawa lakini next time angalia option zote mabichi, storage, processing nk.

Back
Top Bottom