Maundumula
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 7,553
- 3,081
Hongera sana. Mie nakushauri kama kuuza wakati wa kuvuna, uza kidogo sana. Vinginevyo andaa store yakae uuze kuanzia November hadi April mwakani. Vinginevyo nunua au yapeleke mashine za Hill Mapinga saga unga uuze kwenye maduka au sokoni. Ungekuwa mfugaji ndio fursa ya kuyatumia kwa mifugo yako. All the best
Mama Joe,
Tatizo sina pa kuyaweka ningependa niyaweke lakini italeta shida nimepiga hesabu chap chap naweza kuingia gharama kubwa nikikodi eneo.
Kama ni hivyo anza kutafuta soko kwa kina Bakhressa, wenye mashine za kusaga kama huyo Hill inakupunguzia gharama usafiri.
Ila nafikiri uulizie soko la unga ujaribu kusaga na kuuza bila kuhifadhi, mfano ukipata oda kiasi hiki unaongea mashine unasaga unapack na kupeleka. Jaribu option tofauti lakini ukiprocess ndo faida zaidi.
Habari zenu wandugu,
Kwanza nashukuru kwa kunipa hamasa ya kuingia kwenye kilimo.
Inshallah mambo yakienda vizuri nategemea kuwa na mahindi kama gunia 800 au zaidi mwezi wa saba mwaka huu hapo Bagamoyo
Naomba kujua nitauza wapi haya mahindi?, kama wateja wapo ikifika wakati naomba tuwasiliane.
Hayo mahindi kidogo sana, peleka pale sokoni Tandale, usipoteze muda hata kwenda Kariakoo!
Hapo Tandale taratibu zao zipoje?
Mkuu peleka mzigo pale sokoni, majibu utayapata palepale.
Ndiyo nini hiki unachomshauri yaani apakie mzigo apeleke tu bila kujua hata utaratibu?
Soko huria hujui taratibu zake!
kwanini usianze na kuuza mabichi?...
tena kwa bagamoyo to dar hakuna gharama kubwa za usafiri which means
utapata faida kubwa sana waweza uza mabichi kwa sasa NA KIBARIDI HICHI KUNA FAIDA
Nilifikiria wazo la kuyauza mabichi ambayo inafaida kubwa lakini nikasita maana nikianza kuvuna wasije wanakijiji wakasaidia kuvuna zaidi ikaleta shida.
Nilifikiria wazo la kuyauza mabichi ambayo inafaida kubwa lakini nikasita maana nikianza kuvuna wasije wanakijiji wakasaidia kuvuna zaidi ikaleta shida.