SI KWELI Mahinyila asema No reform no election ni mpango wa Lema na Lissu kuchota hela Diaspora na Bavicha watashiriki uchaguzi 2025

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wakuu hii imekaaje kuwa Mahinyila amesema No reform no election ni mpango wa Lema na Lissu kuchota hela Diaspora na Bavicha watashiriki uchaguzi 2025. Je, ni kweli?

 
Tunachokijua
Deogratias Mahinyila ni Mwenyekiti wa baraza la vijana wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA (BAVICHA) Taifa. Mnamo Machi 4, 2025 akiwa na viongozi wengine wa baraza hilo alifanya mkutano na waandishi wa habari ukiwa na lengo la kuongelea hali ya usalama kwa vijana Tanzania, ikiwemo tukio la utekaji lililomkumba katibu mkuu wa BAVICHA mkoa wa Mwanza Amani Manengelo, Februari 14, 2025.

Madai

Kumekuwapo na taarifa inayodaiwa kuchapishwa na Jambo TV ikiwa na kichwa cha habari 'Mahinyila asema No reform no election ni mpango wa Lema na Lissu kuchota hela Diaspora na Bavicha watashiriki uchaguzi 2025.

Uhalisia wa madai hayo

Ufuatiliaji wa kimtandao wa JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (Key Word Search) umebaini kuwa Taarifa hiyo Si ya Kweli kwani Mahinyila hakutoa kauli hiyo, pia haikuchapishwa na Jambo TV.

Aidha kupitia mkutano na waandishi wa habari aliofanya Mahinyila mnamo Machi 04, 2025 ambapo dhima kuu ilikuwa ni kukemea matukio ya utekaji, hakutoa kauli yoyote kuhusu ajenda ya No reforms No election na ushiriki wa vijana uchaguzi 2025.

JamiiCheck inakukumbusha kufanya uhakiki wa kila taarifa unayokutana nayo mtandaoni kwani kumekuwapo na machapisho mengi yakitumia machapisho ya vyombo mbalimbali vya habari mbalimbali vya habari. Tazama hapa, hapa, hapa na hapa, ni taarifa za upotoshaji zilizotumia utambulisho wa Jambo TV.​
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…