Mahinyila: Polisi wanatugonga virungu kwasababu wana stress, CHADEMA hatujawahi kuwa maadui wa Polisi

Mahinyila: Polisi wanatugonga virungu kwasababu wana stress, CHADEMA hatujawahi kuwa maadui wa Polisi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Taifa, Wakili Deogratius Mahinyila amesema hatakuwa tayari kuona wananchi wanaonewa kwa mambo mbalimbali kama kutozwa kodi na kukamatwa na polisi 'kiholela' hivyo atapambana ili kujenga kuheshimiana kati ya wananchi na mamlaka.

Mahinyila amesisitiza hilo tarehe 31 Januari, 2025 wakati akizungumza na wananchi wa Mpwapwa mkoani Dodoma alipokuwa akielekea kijijini kwao Berege ikiwa ni mara ya kwanza kufika huko tangu kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo
 
View attachment 3220845
Ghafla nimempenda huyu kijana na kama kweli tunalo jeshi la polisi naliomba kuzingatia ushauri mnaopewa na kijana kama huyu...kazi yenu ya kwanza ni kumlinda mwananchi na mali zake.

Mnaposhiriki katika uvunjaji wa katiba kwa maagizo ya yeyote yule mjue hamwatendei haki Watanzania ambao kimsingi ndio mabosi wenu wanaowawezesha kuishi na kulisha familia zenu.

Jukumu lenu lingine kulingana na katiba ni kulinda amani na kwa kuwakumbusha tu pasipo na haki hakuna amani na palipo na uonevu hakuna haki hivyo msingi mkubwa wa amani ni haki.

Kwa kumalizia ni kwamba bila haki, hakuna amani...sanasana kuna utulivu tu kwa uvumilivu dhidi ya maumivu, mateso na manyanyaso tunayoyapitia hivyo mkae mkijua kuwa iko siku na haiko mbali!
 
Mapolive wengi wakistaafu ni kisukari, Pressure, Figo, Miguu kuvimba - laana ya uonevu.
 
Polisi wenye akili wanaweza kupata hekima humo kwenye busara za huyo kijana.
 
Sasa hata kama hamna uadui na polisi, pia urafiki na polisi hautakiwi maana wale ni jeshi.

Muhimu Kila upande ujue mpaka wake.
 
Back
Top Bottom